KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova.
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova
leo anatarajiwa kutangaza ripoti ya timu iliyoundwa kuchunguza vitendo
vya uporaji eneo la Kigamboni.
Timu hiyo iliundwa kwa kushirikiana na
wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), ambao hivi karibuni
waliandamana kupinga vitendo vya kudhalilishwa kwenye hosteli zilizopo
eneo hilo.
Maandamano ya wanachuo yalikuja baada ya
udhalilishwa na kulawitiwa kwa mwezao, huku wakidai malalamiko ya
kuporwa, kuibiwa, kubakwa waliyokuwa wakiripoti polisi yalikuwa
hayafanyiwi kazi na polisi.
Januari 14, mwaka huu wanafunzi hao waliandamana
hadi Wizara ya Mambo ya Ndani na baadaye Uwanja wa Machava uliopo
Kigamboni, waliwasilisha malalamiko yao kwa Kova.
Katika maandamano
hayo, polisi walitumia nguvu za ziada ikiwamo mabomu ya machozi na
vipigo kwa wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulelekea Kituo cha Polisi
Wilaya ya Kigamboni.
Polisi waliwasambaratisha huku baadhi yao wakikamatwa, lakini baadaye waliachiwa. Katika
malalamiko hayo, wanafunzi hao wanadai kuibiwa kompyuta ndogo (laptop),
simu, fedha na vitu vingine huku wakidai polisi wanawafahamu wahusika
wakuu wa vitendo hivyo, lakini hawachukui hatua yoyote.
Walidai vitendo hivyo vimekithiri na vimekuwa vikifanyika muda mrefu, huku wahalifu wakifahamika.
Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha IFM
(IFMSO), ulisema hali katika hosteli hizo imekuwa salama, lakini
wanasubiri taarifa ya timu iliyoundwa itakayotolewa leo.
Waziri Mkuu wa IFMSO, Daniel Sarungi alisema
hakuna tukio lolote baya walilopelekewa na wenzao wanaoishi kwenye
hosteli hizo tangu walipoandamana.
Baadhi ya wananchi waishio eneo hilo walisema kuna hali ya amani kiasi tangu walipoandamana.
0 Comments