FUNDI PIKIPIKI ANAYETISHA JIJINI DAR


Na Hassan Haji Ndunda

Kenneth Batega Rusimbi ama kama anavyofahamika kwa wengi kwa jina la KENNY mwenyeji wa Ujiji Kigoma kunakopatikana samaki hadimu wa Migebuka.

Fundi Kenny akii assemble Engine

 KENNY ni fundi pikipiki kubwa nikimaanisha kuanzia 250cc hadi 1500cc na kuendelea na anatengeneza pikipiki za aina tofauti tofauti kama: SUZUKI, HONDA, YAMAHA, KAWASAKI, KTM nk. Fundi Kenny anafanyia shughuli zake katika Mtaa wa Amani na Jangwani karibu kabisa na Jengo la timu maarufu nchini Tanzania ya Dar Young Africans Jijini Dar es Salaam.


Fundi KENNY hadi hivi sasa anauzoefu katika kazi hii kwa takribani miaka ishirini na mitano (25) akiwa pia anasaidiana na mafundi mahiri na wazoefu pia hapa ninawazungumzia Kasongo Abeid na Kiomoni Mbarouk.

Fundi Kasongo Abeid

KENNY si mchoyo wa ujuzi, pia anatoa ujuzi kwa vijana wanaoonyesha hari ya kutaka kufuata nyayo zake, anao vijana machachari katika fani hii nao ni: Ramadhani Mustafa, Maulid Salum, Salum Issa (Lyala) na Hussein Hamidu (Professional) hapa ni kazi tu kwa kwenda mbele.


Endapo ulishasumbuliwa sana na mafundi kwa ajili ya matengenezo ya Pikipiki yako hasa zenye ukubwa kama ilivyoelezwa hapo juu, kama uko Dar es Salaam au uko mikoani basi usisite kumuona Fundi Kenny utapata suluhisho la tatizo lako.


Anapatikana kwa nambari hizi za simu: 0713313376 au 0776313376

Maulid Salum - Fundi Mwanafunzi Amani Fresh Motorcycle


Fundi Mwanafunzi Ramadhan Mustafa Amani Fresh Motorcyle




Fundi Kenny






Karibuni Sana Amani Fresh Motocycle

Post a Comment

0 Comments