MBIO ZA BEACH MARATHON ZAFANA KIGAMBONI 

WASHIRIKI WA RIKA NA JINSIA MBALI MBALI WASHIRIKI MBIO HIZO

Mashindano ya Aina yake ya Beach Marathon yalifanyika tarehe 7 Novemba' 2020 kwa kuwashirikisha washiriki toka sehemu mbali hapa nchini toka Mavyuoni, Taasisi mbali mbali, Makampuni na hata mtu mmoja mmoja na hayakubagua rangi, kabila, umri, jinsia nk. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na BEACH Marathon yenye makazi yake Ungindoni Kigamboni yalipeneza sana kutokana na idadi kubwa ya washiriki.

Mashindano yalianzia katika Beach ya Rongoni Beach Resort Kigamboni hadi South Beach Resort na kurudi tena Rongoni Beach Resort yalipoishia, mbio hizo zilikuwa ni za umbali wa kilomita 15, 10 na 5.

Sehemu ya kuanzia na kumalizia Mbio Rongoni Beach Resort Kigamboni


Washiriki wa mbio za kilomita 15 na 10 wakianza mashindano


























Mshiriki Jofrey Gama akikimbia mbio za kilomita 15


Washiriki wenye vituko nao hawakukosekana, mshiriki huyu aliamua kukimbia mbio kyk vazi la msuli na kanzu fupi

Wadada nao hawakuwa nyuma ktk ushiriki huu wa mbio za Ufukweni



Mashindano haya pia ni sehemu ya utunzaji wa mazingira ya fukwe na kuzifanya ziwe safi na salama. Kama mabango ya hapa chini yanavyojieleza.



" Wakati ujao ukifika tujitokezeni kwa wingi tushiriki ni mazuri na nimeyapenda "  alizungumza mmoja wa washiriki nilipoongea nae

Post a Comment

0 Comments