MAANDALIZI YA HARUSI YA JELLA BEGA NA BI SAFI YAPAMBA MOTO

JELLA BEGA NA BI. SAFI RELAXING TIME

Maandalizi ya Harusi ya Wawili wanaotarajia kufunga pingu za Maisha siku ya jumamosi ya tarehe 8 Novemba' 2014 yameendelea kupamba moto baada ya Kamati maalum ya maandalizi ya Harusi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti Mahiri katika mambo ya kuweka sawa na kuhakikisha katika sherehe hii inafanikiwa na kufana Godfrey William Mahende akisaidiana na Katibu wake asipenda mambo yaharibikie mlango si mwingine ni Mr. Gabriel Magessa.


Sherehe hii pia inatarajia kuongozwa na MC Mahiri anayekwenda na muda na wingi wa burudani si maneno pekee namzungumzia MC CHIPOLOPOLO. mziki wake utauona siku ya siku ikiwadia.


Katika kudhihirisha kuwa sherehe imepangwa na kupangika safu ya walinzi na wasimamizi wenye fani kibao za kusimamia sherehe utakutana na Bestman Mr. Mario Philipo Nyalusi na Matron Bi. Jesca.


Kama kawaida HVP Studio tutawajibika katika kushughulikia suala zima la kumbukumbu za picha za kutembea namaanisha (Video) na za mnato yaani (Still picture) chini ya usimamizi wa Super Editor & director Hassan haji Ndunda na Crew yake ya Haji'z Video Production.















Post a Comment

0 Comments