BJ THE DON (SELE) KUJA NA NGOMA KALI IITWAYO "NIKUPIGIE NGOMA MARIMBA"

BJ THE DON (SELE)

Msanii Chipukizi wa Bongo Fleva na Miandoko ya Bongo Fleva Bolingo Sele aka BJ The DON kama anavojulikana kwa mashabiki wake walioko katika Jiji la Dar es Salaam pande za Magomeni na Jiji zima la Dar es Salaam bila kuisahau baadhi ya mikoa hapa nchini Tanzania.

BJ THE DON


Anatarajia kuipua Kichupa chake kikali kinachokwenda kwa jina la "NIKUPIGIE NGOMA MARIMBA UCHEZE" ilioko katika miondoko ya Bongo Fleva Bolingo. kazi nzima ya kuiandaa, kushuti na Editing ya kichupa hicho imeshafanyika na imekamilika na muda wowote inatarajia kusambazwa katika vituo vya Luninga.


BJ The DON amekuja kivingine baada ya kulisoma soko la muziki lilinyokaa na kuamua kutoka kiaina, ni nyimba nzuri na kazi nzuri pia iliyofanywa na HVP Studio (Haji'z Video Pro) katika kukigonga kichupa hicho na editing ya kufa m2.


Ngoma imekaangwa kiuhakika na Producer anayekuja juu kama Gesi ya Mtwara naye si mwingine bali ni NASCOBA toka katika Studio yake mahiri ya PATA RECORD yenye maskani yake kule katika viunga vya Mabaibo.

NASCOBA


Video imebebwa na Madada mahiri katika kuzizunguusha nyonga nao ni Video Queen Bibie Mariam, bila kumsahau mzungusha kiuno mithili ya mapanga boi ya helikopta hapa namzungumzia Da Queen Mmmmmh! huu ni moto wa kuotea mbali katika Video hii. na pia utakutana na mwanadada nayejua kuzicharaza drums si mwingine ni Trisa Queen.

Queen


Director katika video alisimama Mzee mzima anayecharuka na kazi zake bila maskhara Hassan Haji Ndunda toka Kampuni ya HVP Studio (Haji'z Video Pro) iliyopo Kigamboni Dar es Salaam. ambayo pia iko bize kwa sasa ikivipika vichupa tisa vya nyimbo za gospel katika album ya "USIJIDHARAU" ya Rev. Petro Mwanenuka ambazo zitakamilika mwishoni mwa mezi huu.

TRISA QUEEN


Fuatilia Blog hii baada ya wiki tu kichupa hicho kitakuwa  angani.

Post a Comment

0 Comments