![]() |
Wastara na Marehemu Sajuki kulia |
![]() |
Juma Kilowoko "Sajuki" na Wastara siku ya Ndoa yao |
Mwigizaji Dinno alikua rafiki mkubwa sana wa Marehemu Sajuki na ndio alikua analala hospitali na Sajuki pale Muhimbili.
![]() |
Aliyekuwa rafiki mkubwa wa karibu wa marehemu Sajuki - DINO |
Ameongea AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na kutoa maneno ya mwisho ambayo aliyasikia kutoka kwa Sajuki akimzungumzia mke wake ambae ni Wastara.
Kwa haraka haraka mwigizaji Wastara amesifiwa sana na watu mbalimbali kwa moyo wake wa ushujaa wa ukweli wa upendo kwa Sajuki japo walipitia matatizo makubwa na mengi kwenye maisha yao.
Yusuf Mlela kushoto na Marehemu Sajuki kulia walipokwenda kuwatembelea watoto Yatima Mwanza |
Masanja Mkandamizaji na Arnold
Kayanda ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania waliopaza sauti zao kupitia
mitandao ya kijamii kumsifia Wastara kwa moyo wa upendo.
![]() |
JB kushoto akiteta jambo na Baba Mzazi wa Sajuki Mzee Kilowoko |
Tukirudi kwa Dinno, namkariri
akisema “tulipokuwa Arusha sisi watatu tu Sajuki alionyesha ishara ya
kukata tamaa, siku moja tulikua hotelini usiku kama saa tisa hivi
Wastara alikuja kuniamsha kwenye chumba changu nikaenda kwa Sajuki,
alikua anaumwa sana akamwambia Wastara naomba mpigie mama niongee nae,
Sajuki akamwambia mama yake mzazi kwamba Wastara nampenda sana,
kanizalia mtoto mzuri anaitwa Farhini, naomba msimsumbue naomba msimpe
shida yoyote amenisaidia sana, naomba mumwachie Farhini amlee amtunze
mtamuona, yalikua maneno mazito sana mpaka machozi yakawa yananitoka”
![]() |
Mama mzazi wa SAJUKI akilia kwa uchungu kufuatia kifo cha mwanae |
Mbali na hayo, Dinno
amesema jambo jingine ambalo Sajuki aliliongea mwishoni ni kuhusu upendo
miongoni mwa wasanii wa movie Tanzania, namkariri akisema “alikua
ananiambia hebu jitahidi kuwa unakaa na wasanii, unajua sisi hatupendani
Dinno ila mimi iko siku nitakuja kuropoka nikae na watu niwazungumzie
tuweke upendo pamoja, tukishapendana tutafanya kitu Dinno”
0 Comments