TASWIRA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA MWIMBAJI WA TOT TAARAB MAREHEMU MARIAM KHAMIS


 Marehemu Mariam Khamis enzi za uhai wake




Huu ndio usafiri wetu wa mwisho pindi tuondokako duniani ambapo dada yetu Mariam Khamis ameutumia siku ya leo kuelekea makaburini




Mamia ya watu walijitokeza katika mazishi ya muimbaji mahiri wa Taarab nchini Mariam Khamis maarufu kama Paka Mapepe aliyefariki juzi wakati akijifungua. Mariam alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo mtoto wake alisalimika.

Mazishi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu wa aina mbalimbali wakiwemo wasanii wengine wa muziki wa Taarab.

Miongoni mwa wasanii waliohudhuria mazishi hayo ni pamoja na Khadija Kopa, Isha Mashauzi, Omari Tego, Ally J, Capt Temba toka Fungakazi Modern Taarab, Msanii Mboto na wengineo toka tasnia ya Filamu, Mzee Yusuph na mke wake Bi Leila, Nyota Waziri, Bi Hindu na wasanii wenzake wa kundi la TOT na wasanii wengine toka makundi ya Taarab na wengineo wengi walioshiriki si rahisi kumtaja kila mmoja.




 Mwili wa marehemu Mariam Khamis ukiwa unaelekea makaburini mapema leo



 Mamia ya watu walio jitokeza kumsindika dada Mariam kwenye nyumba yake ya milele



 Mume wa marehemu Mariam Khamis akiingia ndani ya kaburi tayari kwa kumzika mkewe pembeni yake ni baba mkwe wake



 Tayari kwa kupokea mwili wa marehemu pindi uingizwapo ndani ya kaburi



 Mwili wa marehemu Maraiam Khamis ukiingizwa ndani ya kaburi



 Mazishi yakiendelea ndani ya kaburi



 Tayari dada Mariam kashazikwa hapo zoezi la kufukia na mchanga likiendelea



 Mwanamuziki wa Taarab Thabit Abdul naye akiiendelea na zoezi la kufukia kaburi la dada Mariam Khamis



 Na hii ndio nyumba yake ya mwisho dada Mariam Khamis ambayo ataishi maisha yake yote



 Kaburi la marehemu dada Mariam Khamis likiwa katika muonekano ambao tayari lishafukiwa




Mume wa marehemu Mariam Khamis akiwa haamini kuwa mkewe hayuko naye tena duniani kiukweli alichokuwa akikiongea hapo pembeni ya kabuli ungekuwepo wewe rafiki yangu sidhani kama ungeweza kuvumilia lazima ungelia pole sana kaka HAJI KIJUNGU mbele yake nyuma yetu.



Mume wa marehemu Mariam Khamis aliporudi nyumbani tu kutoka makaburini alimtafuta mwanaye huyo mtoto unayemuona mwenye tisheti yenye mistari alipomuona tu akaangusha kilio cha nguvu. Mungu awatie nguvu.

---

Mariam alikuwa muimbaji wa kundi la taarab la TOT na enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab ambayo ni pamoja na East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.

Marehemu Mariam Khamis ameimba nyimbo nyingi zinazofanya vizuri katika muziki wa Taarab zikiwemo ‘Huliwezi bifu’, ‘Raha ya Mapenzi’ na ‘Ndo basi tena’.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pepa peponi.

 

Picha zote kwa hisani ya CHIMBUKO LETU BLOGSPOT

Post a Comment

0 Comments