LOS ANGELES, Marekani
WAKATI wanawake wengi duniani
wakihangaika kukuza ukubwa wa makalio yao, huku wengine wakitumia njia
ya kuvaa taiti zenye hipsi, wanaume wengi huko mjini Los Angeles
wamejikuta wakigeukageuka kumwangalia mwanamke mwenye makalio makubwa
kupita kiasi kila apitapo njiani.
Mikel Ruffinelli ni mwanamke ambaye mpaka sasa
‘ameishavunja shingo’ za wanaume wengi. Makalio yake na hispi zake za
asili zimemfanya atawazwe kuwa mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko
wanawake wote duniani.
Mikel anayeishi nchini Marekani hajatumia dawa za
mchina wala dawa zozote kama wafanyavyo akina dada wengine na ndiye
aliyetambulishwa kuwa ndiye mwanamke mwenye hipsi kubwa kuliko wanawake
duniani. Mpaka sasa mama huyo mwenye familia yake ana hispi zenye mita
2.44.
Umbile lake halikuja hivihivi, bali alikuwa ni mtu
mwenye umbile la kawaida, licha ya kukiri kuwa ndugu zake wengi wana
maumbile makubwa.
Hipsi za mwanamama huyo zimekuwa zikiongezeka siku baada ya siku kadiri alivyokuwa akijifungua watoto wake.
Mikel Ruffinelli, ambaye ni mama wa watoto wanne
ana umri wa miaka 39 na ni mkazi wa Los Angeles amejisifia kuwa umbile
lake limekuwa likiwachanganya wanaume wengi.
Akiwa na kiuno kidogo kisichoendana na mwili wake cha inchi 40, hispi zake zina mzunguko mkubwa wa inchi 96.
“Nalipenda
umbile langu na sina mpango wa kujikondesha kwa diet,” alinena Mikel na
kuongeza kuwa wanaume wengi wanapenda wanawake wenye maumbile makubwa
siyo wale wembamba wembamba.”
Lakini kauli hiyo, imepingwa vikali na Jennifer
Lopez, Kim Kardashian na Beyonce ambao wanasema inategemea na mwanaume
husika na namna kile anachokipenda, lakini wakati mwingine hutegemea na
mazoea ya mwanamume.
Mikel pamoja na kutamba na maumbile yake hayo
ambayo anadai ni urithi toka kwenye familia yake ambapo karibuni ndugu
zake wote wa kike nao wana hispi kubwa.
Mikel amelazimika kuishi tofauti ili aweze
kuendana na umbile lake, hawezi kuenea kwenye gari ndogo hivyo gari
analoliendesha ni kama lori.
Akiwa nyumbani kwake inabidi akae kwenye makochi
yaliyotengenezwa kwa chuma badala ya mbao, pia kitanda chake nacho ni
futi saba kwa saba.
Mume wa Mikel, Reggie Brooks mwenye umri wa miaka
40 ameelezea kupagawishwa na umbile la mkewe na ameongeza kuwa kila siku
humsifia kwa kumwambia jinsi gani alivyo mrembo.
Mikel na mumewe wapo kwenye ndoa kwa miaka 10 sasa
na wamefanikiwa kupata watoto watatu ambapo mtoto wa kwanza wa Mikel
alizaliwa katika ndoa yake ya kwanza kabla hajaachika na kuolewa na
Reggie.
0 Comments