CAPT TEMBA: "NIMEJIANDAA KISAWASAWA"

Mkurugenzi wa Fungakazi Modern Taarab Karia almaarufu Captain Temba (Mchaga wa Kwanza kuimba Taarab nchini Tanzania)

KARIA TEMBA al-maarufu Kapteni Temba Msanii anayekuja juu hivi sasa katika fani ya muziki wa Mwambao (Taarab) hapa nchini, akiwa ndiye Mkurugenzi anayesimamia kundi zima la FUNGAKAZI MODERN TAARAB na yeye pia akiwa ndiye mtunzi mkuu.


Kapteni Temba baada ya kutamba na album yake ya Fungakazi yenye nyimbo kama "Nimeiteka Himaya" alioutunga na kuuimba yeye mwenyewe, ukifuatiwa na "Usisemwe kwani wewe Nani" Mtunzi Capt Temba, umeimbwa na Capt Temba na amemshirikisha msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) kijana mwenye sauti adimu Z Anto na ambaye amefanya vizuri sana katika wimbo huu.

Rahma Machupa na Detective Senior Bachelor

mbali na hizo pia kuna wimbo uitwao "Mambo yangu yanawahusu nini" mtunzi capt Temba na umeimbwa na mwanadada (Red Beauty) Ashura Machupa, wimbo huu ni moto wa kuotea mbali. na wa nne unaohitimisha na kubeba album ya Fungakazi ni wimbo uitwao "Fungakazi" uliotungwa na kutiwa mashairi na Kapteni Temba na kuimbwa na wadada watatu (Mapacha watatu) Machupas Family hapa tunamzungumzia Rahma Machupa ambaye kwa sasa yupo Jahazi, Zainabu Machupa na Red beauty Ashura Machupa. Nyimbo hizi zote zipo hewani namaanisha redioni na kwenye Luninga mbali mbali ndizo zinazokimbiza kwa sasa.

Kutoka kushoto Zainabu Machupa na Red beauty Ashura Machupa

Katika mahojiano na blog hii, Kapteni Temba amesema kwamba kwa sasa anakuja na nguvu mpya na staili ya kubamba chati kwa vibao vyake vitatu vikali wa kwanza unaitwa "INZI WA KIJANI" taratibu zote za kuufyatua zimekamilika utakaoimbwa na Red beauty Ashura Machupa, Zainabu Machupa na mwanadada Hanifa Maulid (Jike la Chui) toka Kings Modern Taarab, wimbo mwingine utakaopakuliwa utaimbwa na kijana Detective Senior Bachelor yeye atashuka na kibao kisemacho "SWEET LANGUAGE" hapa pana uhondo usiostahili kupitwa na haya mambo.

Malkia wa Mipasho Afrika Mashariki na kati Khadija Omari Kopa

Mbali na hizo Capt Temba atashusha kibao kingine kiitwacho "HAKUNA KABURI LA MJINGA" mtunzi wake mwenyewe na hapa amemshirikisha Nguli wa Mipasho ya Pwani, Malkia wa mipasho afrika Mashariki, Hondohondo mlezi wa wana huyu si mwingine ni Malkia Khadija Omari Kopa, wimbo huu umesheheni mashairi yenye vina na mipasho ya kushibishwa ni hot chill, wapenzi wa Fungakazi Modern Taarab na Malkia Khadija Omari Kopa kaeni mkao wa kupakuwa kazi zote za shooting za video za nyimbo hizi zitafanywa na HVP STUDIO chini ya Mkurugenzi wa HVP Studio Hassan Haji Ndunda na Director Salum Diva Sasamalo na kijana Detective Senior Bachelor  "MOTO NA BURUDANI WAJA"


Post a Comment

0 Comments