Maharusi Bw. Batholomeo na Cecilia muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika Kanisa la St. Peter Oysterbay Dar es Salaam |
Hayawi Hayawi leo yametimia baada ya mipango ya muda mrefu ya Harusi kati ya Bwana Batholomeo Ngoti Mtun'ge na Bibi Cecilia Dembe kukamilika leo tarehe 29 Septemba' 2012 katika Kanisa la St. Peter Oysterbay jijini Dar es Salaam walipopanda kwenye madhabau ya bwana na kufunga ndoa takatifu iliyohudhuriwa na ndugu, marafiki na jamaa wa karibu na kisha tafrija yake ikahitimishwa pale katika ukumbi wenye viyoyozi yaani (Full Kipupwe) wa Deluxe Social Hall Sinza jijini Dar es Salaam.
Sherehe ilijaa shanrashamra kibao nderemo na vifijo vilitawala kila wakati katika mtindo wa aina yake wa ushangiliaji uliobuniwa na MC Mahiri huyu si mwingine namzungumzia Dada Luciana MC aliyeichangamsha sherehe na kuifanya ichangamke sana.
Sherehe hii pia mbali na kuhudhuriwa na watu mbali mbali maarufu, pia ilihudhuriwa na wasanii kadhaa akiwemo Mzee Magali nguli wa tasnia ya filamu nchini Tanzania, Msanii wa sauti kibao na zinazoburudisha na kuchekesha kiasi cha kuwafanya wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hii kushikilia mbavu zao aitwaye Mrugaruga, na bila kuwasahau waburudishaji kupitia nyimbo za Injili.
HVP Studio inaipongeza Kamati ya Harusi kupitia kwa kiongozi mkuu Mwenyekiti Mr. Benard Ngulika kwa kuongoza vyema na kufanikisha sherehe hii. pamoja na wajumbe wake na viongozi wake bila kumsahau Katibu Mr. Norbert Nongwa, Makamu Mwenyekiti Mzee Augustino Kalinga na Watunza fedha Mr & Mrs Romanus Mtung'e
Patron na Mtron wakiwa Kanisani St. Peters Oysterbay Dar es Salaam |
Maharusi wakila kiapo cha ndoa St. Peters Oysterbay Dar es Salaam |
Batholomeo na Cecilia mbele ya Madhabau ya Bwana St. Peter Oysterbay Dar es Salaam |
Shamrashamra nje ya kanisa mara tu baada ya kufunga ndoa |
Mbalamwezi Beach Mlalakua |
Mbalamwezi Beach Mlalakua |
Bi. Harusi Cecilia na Wapambe Mbalamwezi Beach Mlalakua |
Kaka Mkubwa wa Bwana Harusi ndani ya Ukumbi wa Deluxe Sinza |
Maharusi, Patron na Matron wakifungua Champagne ndani ya Ukumbi wa Deluxe Sinza |
Bibi Harusi Cecilia Dembe |
Bw Harusi Batholomeo Ngoti Mtung'e |
Matron |
Patron |
Katibu Mr. Norbert Nongwa |
Mr. Romanus Mtung'e akikabidhi zawadi ya jadi sengo na Jembe kwa Maharusi |
Kamati ya Maandalizi wakitoa mkono wa pongezi kwa maharusi |
0 Comments