Rais Jakaya Kikwete, leo anatarajiwa kukabidhi nyumba 36 kwa waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck
Sadiki, Rais Kikwete atakabidhi nyumba hizo zilizojengwa na Serikali
katika maeneo ya Msongola Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.
Sadiki alisema makabidhiano hayo yatafanyika katika maeneo hayo kuanzia mchana.
Februari 18, mwaka jana, ilitokea milipuko ya mabomu katika kambi ya
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) iliyoko Gongo la Mboto na
kusababisha vifo vya watu takribani 30 na wengine 600 kujeruhiwa.
Watu kadhaa walikosa makazi baada ya nyumba zao kuharibiwa.
Taarifa ya tathmini ya athari za nyumba ilionyesha kuwa nyumba 77 ziliharibika kabisa na 1,748 ziliharibika kidogo.
0 Comments