Sue Noel akiwa na mumewe Noel na baadhi ya watoto wao,wakati wakihojiwa
na gazeti la Uingereza la Dailymail,mama huyo mwenye watoto 16 bado
anatarajia kuongeza wengine.
LANCS, Uingereza
MWANAMAMA aliyekuwa anaongoza kwa kuwa na watoto
wengi jijini London, Sue Noel amejifungua mtoto wake wa 16, lakini hata
hivyo amesikika katika vyombo mbalimbali vya habari jijini humo akisema
kuwa anataka kuongeza watoto wengine zaidi.
Sue baada ya kujifungua mtoto wake Casper, alipokelewa na sherehe kubwa ya mila za nchini Uingereza kutoka kwa familia yake.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 37 ambaye
alikuwa akiishi katika nyumba ya zamani na familia yake na isiyo na
huduma alisema, “Ninafurahia zaidi kuwa mama. Sisi tuna bahati sana.”
Sue
awali alipata ujauzito akiwa na umri wa miaka 14. Yeye na mumewe Noel,
ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 41, walifanikiwa kupata mtoto wa
kwanza aliyeitwa Chris ambaye kwa sasa ana miaka 23 na walipewa huduma
zote wakati wa kuzaliwa kwa mtoto huyo.
Wapenzi hao walioana baada ya Sue kutimiza umri wa
miaka 18 na hivi sasa Sophia ana miaka 18 ambaye ni mtoto wa pili
aliyezaliwa mara tu baada ya ndoa, baadaye alizaliwa Chloe (17), Jack
(15), Daniel (13) na Luke mwenye miaka 11 sasa.
Millie (10), Katie (9), James (8), Ellie (7),
Aimee (6), Josh (4), Max (3), na Tilly May mwenye miaka miwili
anayefuatiwa na Oscar ambaye alizaliwa Oktoba 2011 kabla ya Casper
ambaye kwa sasa ni mchanga aliyezaliwa wiki tisa zilizopita.
Sue ambaye anafanya kazi ya kuwaendesha watoto
kutoka shule kwenda nyumbani katika basi alisema, “Ninayaona hayo yote
kama ndoto.”
“Ninapata mhemko sana ninapowaona watoto pamoja.
Najua watu wanaona ajabu. Wapo wengine wanaodhani kwamba watoto
hawatapata matunzo yanayostahili, hawatambui ni namna gani sisi
tunajitolea katika hili. Labda tunaweza kuwa na bahati kwa kuwa na
watoto wengi zaidi.”
Familia inatumia zaidi ya Paundi 250 sawa na Sh625,000 kwa ajili ya chakula kwa muda wa wiki moja.
Kila siku wao wanamaliza mikate mitatu, masanduku
mawili ya unga na pakiti 18 za maziwa. Kwa makadirio ya wastani
wanatumia pakiti 16 za nyama zilizoandaliwa na mboga zenye uzito wa kilo
5, kabichi tatu na karoti 30.
Nyumba wanayoishi ina vitanda tisa kwa ajili ya
watoto tu huko Morecambe, Lancs. Nyumba hiyo ina mashine kubwa kwa ajili
ya kufulia nguo na friji kubwa.
Familia hiyo kwa sasa imekuwa kwani licha ya Sue
kutangaza kuwa bado anahitaji kuendelea kupata watoto, tayari binti
yake, Sophie ambaye alizaliwa na Sue na Noel ana mtoto aitwaye Daisy.
Herieth Makwetta kwa msaada wa mtandao
0 Comments