HARARE, Zimbabwe
MFANYAKAZI za ndani ‘hausigeli’ amehukumiwa
kifungo cha miezi miwili jela na viboko, kwa kosa la kumnywesha mkojo
bosi wake kutokana na hasira ya kutolipwa mshahara wake kwa wakati.
Rita Chakwesha mwenye umri wa miaka 25, ambaye
aliajiriwa katika nyumba iliyopo kwenye Barabara ya Avenue mjini Harare,
kwa makusudi alimnywesha mwajiri wake Sharlotte Chivavarirwa maji
yaliyokuwa na mkojo ndani yake.
Chakwesha alionekana mbele ya Hakimu Barbra
Masinire huko Harare, akihukumiwa kwa makosa hayo, huku akijitetea kuwa
alikuwa akifanya hivyo kutokana na kutopewa ujira wake kwa miezi miwili.
Mshauri wa Jimbo la Francesca Mukumbiri aliiambia
mahakama kuwa Novemba 5 majira ya saa 11 jioni, Chivavarirwa alirejea
nyumbani akitokea kazini, na mara baada ya kufika alimwomba msichana
wake wa kazi Chakwesha ampe maji kutoka katika jokofu.
Chakwesha
alienda na kumiminia maji ambayo tayari alikuwa ameyatia mkojo na kumpa
bosi wake kwamba ayafurahie kwani ni maji yaliyokuwa na ladha nzuri.
Mama huyo mwenye nyumba baada ya kufungua jokofu
aliona glasi yenye kitu chenye rangi ya manjano na harufu mbaya, hivyo
akahisi kuwa huenda ni mkojo.
Hata hivyo, Chakwesha hakuishia hapo,
alijikuta akitoa siri kwa rafiki wa karibu na Chivavarirwa, ambaye
hakutaka kuitunza siri ile.
Rafiki huyo alikwenda kumweleza hali halisi
Chivavarirwa ambaye aliamua kulipeleka suala hilo chini ya sheria na
hivyo Chakwesha alikamatwa.
Kabla ya kuburutwa mahakamani, Chakwesha alikiri
kutenda kitendo hicho cha ajabu na kwamba hali hiyo ilitokana na mwajiri
wake kutomlipa ujira wake “Ndanga ndabatwa nemweya wehutsinye,”
Chakwesha aliiambia mahakama.
Herieth Mawkwetta kwa msaada wa mtandao
0 Comments