Mhitimu Ms. Almar (Najma) Abdallah Maganga
Ni furaha ilioje kwa Bi.
Almar (Najma), Wazazi ndugu na jamaa kwa Binti huyu kufikia hapa
alipopafikia leo kwa kupata shahada yake ya kwanza katika Taasisi ya
Ustawi wa Jamii pale Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Kwa
haraka haraka kitu Shahada kwa wale waliozaliwa katikka mikondo ya
Elimu ni suala dogo, lakini kwa familia zingine mtoto au Binti kusoma
hadi kufikia kama alivyofikia Almar ni Inshu na ni bonge la mjanja.
Elimu kwa vizazi hivi vya sasa ina changamoto kibao, mtoto wako
anapofikia katika levo hii hatuna budi kumpa sapoti ya shangwe na
vigelegele kwani si kazi ndogo na rahisi.
Kama
sikosei Almar kwa siku ya Leo tarehe 21 Disemba' 2012 amesogeza sivii
zake na kusonga mbele amejipatia "Bachelor In Social Work" si haba,
jamani ndugu, marafiki na watoto wengine kama kina Gaitani, Auni,
Kachiluu, akina Hamimu, Mzee Mzima Dullah na wengineo huko mliko vuteni
stocking mpaka magotini shughuli iwe shughuli. Sina shaka na Dada zake
waliotangulia kama Naila Kalembo na wengineo waliofagia njia mpaka Almar
kapata kupita bila umande.
Hongera
sana Almar, wazazi Bw na Bibi Abdallah Maganga, Mama Mkubwa Mrs. Santa
Kalembo, Mama Mdogo Mrs Miriam Aziz kwa Sapoti kubwa. Na pia shukrani za
pekee ziwaendee wote walioshiriki katika Congratulation Party pale Mtaa
wa Ngorongoro Chang'ombe Dar es Salaam kwa Sapoti mbali mbali bila
kuwasahau majirani, Dada zake Shufaa, Amina Mnyingi na wengineo kibao si
rahisi kumkumbuka kila mmoja.
Ebu chungulia mustakabali mzima wa sherehe japo kwa uchache tu:
|
0 Comments