Rais Barack Obama (kulia) na mpinzani wake Mitt Romney
LEO ni siku muhimu kwa Wamarekani kwani wapiga kura
wa Marekani wanatarajia kuhitimisha zoezi la upigaji kura katika majimbo
yote ili kumpata mshindi katika uchaguzi wa urais ulio na ushindani
mkubwa.
Rais wa Marekani Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney siku ya
jumatatu walifanya kampeni za dakika za mwisho kwa wapiga kura katika
majimbo muhimu ikiwa imebakia siku moja kabla ya uchaguzi katika juhudi
za mwisho kuvunja ushindani. Katika majimbo ya wisconsin , rais Obama
alimshutumu bwana Romney kwa kujaribu kurejesha mawazo mabaya aliyoyatoa
kabla na kusema taifa haliwezi kufanikiwa bila kuwa na daraja la kati
lenye nguvu.
Kwenye mkutano wa jana asubuhi katika jimbo la kusini la Florida
bwana Romney aliwaambia wafuasi wake kwamba kiongozi huyo aliyoko
madarakani Mdemocrat ameshindwa kutekeleza ahadi zake wakati aliposhinda
kiti cha urais mwaka 2008.
Wananchi wapiga kura nchini Marekani leo wanaelekea kwenye vituo vya
kupigia kura katika uchaguzi huo wa Rais huku wagombea, Rais Obama wa
chama cha Democrat na Mitt Romney kutoka chama cha Republican wakichuana
vikali katika majimbo yanayojulikana kwa Pendulum (Swing States) ambayo
ndiyo yanayotarajia kutegua kitendawili cha mchuano huo.
Rais Obama mwenye umri wa miaka 51 na mpinzani wake Romney mwenye
umri wa 65 wanazidiana kidogo kwa mujibu wa maoni yanayochapichwa na
vyombo vya habari. Katika uchaguzi wa rais wa mwaka 2000, mgombea wa
Democrat alimshinda Bush wa Republican kwa karibu kura 500, lakini Bush
alikuwa rais kutokana na kupata kura 271 za Electoral College
ikilinganishwa na 266 za mgombea wa Democrat.
Ili kushinda katika uchaguzi huu mgombea analazimika kujikusanyia
kura za electoral Collage zisizopungua 270 na tayari Obama
amejikusanyia kura 237 wakati mpinzani wake Romney akifikisha kura 206.
Kitendawili kimesalia katika majimbo ambayo wapiga kura wake bado
hawajashawishika yanayoshikilia kura 95.
0 Comments