MGOGORO wa kugombea nani ni mmiliki wa Ziwa Nyasa
kati ya nchi za Tanzania na Malawi umezidi kuwa mgumu baada ya kushindwa
kuafikiana tena leo kati ya kikao cha mawaziri wa nchi hizo mbili
pamoja na wanasheria wao.
Kutokufikia mwafaka huku kumejitokeza leo baada ya kikao hicho hivyo
pande zote kukubaliana suala hilo liende kuamuliwa na jopo la marais
wastaafu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika
(SADC). Hata hivyo Tanzania imesema endapo SADC watashindwa kutatua
suala hilo litapelekwa tena katika Mahakama ya Usuluishi wa Migogoro
Kimataifa ili haki ipatikane.
Mvutano huo umeibuka zaidi pale nchi ya Malawi ilipoanza kuingiza
makampuni ya utafiti wa mafuta na gesi ambayo yaliingia na kuweka kambi
hadi maeneo ya Tanzania. Tanzania imekuwa ikiamini ziwa hilo ni miliki
ya nchi hizi mbili, huku Malawi ikipinga na kutaka itwae ziwa lote.
0 Comments