Mkazi wa Kenya katika mji wa Kisumu akiliweka gurudumu la gari katika
moto uliowashwa na kuziba njia wakati wa maandamao ya kupinga mauaji ya
aliyekuwa anatarajiwa kugombea Ubunge kwa tiketi ya ODM Shem Onyango
Kwega .Picha na AFP
RAIA wa Kenya jana walifanya maandamano
makubwa kwenye mji wa magharibi ya Kenya ya Kisumu, kufuatia mauaji ya
mwanasiasa wa eneo hilo.
Upingaji wenye vurugu ulizuka siku ya Jumatatu
baada ya, mgombea ubunge Kisumu Shem Onyango Kwega kuuliwa na watu
wenye silaha wasiojulikana wakati alipokuwa anaendesha gari mjini akiwa
na mke wake.
Kwega, mwenyekiti wa tawi la eneo hilo la chama
cha Orange Democratic Movement (ODM) cha Waziri Mkuu Raila Odinga,
alipigwa risasi ya kichwa na baadaye kufariki hospitalini.
Huku Mke wake naye akipigwa risasi na kupelekwa hospitali na watu hao hao waliobainika kumuua mgombea huyo.
Mauaji hayo mwanzoni yalihusishwa na majambazi, lakini sababu za kisiasa hazikutolewa mara moja.
Polisi walifyatua mabomu ya kutoa machozi wakati
mamia ya vijana walipokusanyika katika eneo la mtaa wa vibanda wa mji
huo, lililoko kilomita 350 magharibi ya Nairobi.
"Kikundi kilikuwa kinajaribu kuandamana mjini,"
alisema mkuu wa polisi wa mkoa Joseph ole Tito. "Hatutawaruhusu kuja na
kusimamisha biashara mjini."
Siku ya Jumatatu, watu watatu walifariki wakati
mkebe wa bomu la kutoa machozi lililorushwa katika kioski ambako
walikuwa wakijificha kiliposhika moto na mtu mwingine aliuawa baada ya
kupigwa risasi.
"Kwa kweli hatujui ni nini hasa kilitokea vifo vyote hivi vitachunguzwa kwa undani," Tito alisema.
Chama cha ODM kilitoa taarifa ya kulaani "mauaji
hayo ya kikatili" na kuwataka viongozi kuchunguza sababu" zinazohusiana
na mauaji hayo.
Watu waliofanya uhalifu huo inadaiwa kwamba
walikuwa katika pikipiki ambapo walipomaliza kile walichokitaka
walikimbia na kutokomea mbali kabisa.
0 Comments