“Wanawake hao huvutia biashara kwa
kuwatoza wateja wao Sh1,000 kwa anayependa kushika maziwa na Sh1,500
hadi 10,000 kwingineko na kitendo kikamilifu huwa ni makubaliano na
huanzia Sh 10,000 na kuendelea.”
JUHUDI na harakati za kuzungumza na mwanamke
kiongozi wa kundi hilo hazikuwa rahisi. Ilikuwa lazima kwetu
kujitambulisha kuwa tunatoka taasisi binafsi ya kusaidia wanawake.
Kiongozi huyo, Mama Nasra anasema yeye na mabinti
zake hao, wapo hapo kwa ajili ya biashara nyingi, kwanza ni gongo,
bangi, sigara na ‘mengineyo’.
Anasema baadhi ya binti zake hawafanyi biashara
hiyo kwa njaa, kwani wapo waliotoroka majumbani kwao ambako walikuwa
wakisoma na kupewa mahitaji yote muhimu.
“Kwa wengine hiki ni kipaji tu au hulka. Hao watoto wengine walikuwa wanasoma. Wanapenda wenyewe kufanya kazi hiyo,” anasema.
Anaongeza kuwa hata yeye si maskini na anamiliki
nyumba ya vyumba vitano na sebule maeneo ya Mbagala Rangi Tatu, mali
ambayo ameipata kwa biashara hizo hizo.
Kuhusu kuuza gongo, anasema anaona pombe hiyo, pamoja na bangi vina faida zaidi kuliko bia.
Anasema alishawahi kujaribu biashara ya kuuza bia,
lakini hakuona faida ukilinganisha na faida anayopata kwa kuuza pombe
za kienyeji.
Akiwa ameshika pakiti ya sigara, mwanamke huyo
anaeleza kuwa anawalea wasichana hao na wanashiriki pamoja katika
kufanya biashara.
“Halafu sisi si wakaaji hapa, siku mbili tatu
tunahamia kambi nyingine, umeshanisoma,” anasema huku akiendelea
kuchomoa sigara na kuwapa wateja wake.
Wakati tukiendelea kuzungumza, binti mmoja mweupe
ambaye anaonekana amelewa anaelekea katika shamba la mahindi na mwanaume
aliyeketi naye awali.
Hata hivyo, mwanamke huyo anawazuia wasichana wake kuzungumza lolote na kuwaamuru waondoke katika eneo hilo mara moja.
Anasema: “Si unawaona hao, ‘wamepinda’, hao usiwaone hivyo, wameshashindikana makwao,”
Kwa upande wao, vijana walionipeleka eneo hilo wananihakikishia kuwa huo ni mchana tu …usiku mambo huwa moto zaidi.
0 Comments