ULE UZINDUZI WA ALBUM YA NYIMBO ZA INJILI ULIOKUWA UKISUBIRIWA KWA MUDA MREFU. ZA Rev. Eliah Mwakibete Sasa utafanyika tarehe 4 Novemba siku ya Jumapili katika Ukumbi wa PAMO BEACH RESORT ulliopo Kigamboni Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utasindikizwa na Wasanii kibao wa nyimbo za Injili na Kwaya mbali mbali pia zitahudumu. mbali na hayo mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mh. Ezekiel M. Gwatengile toka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Sherehe hizo za uzinduzi wa Album ya USIWE KAMA KIBAO unatarajiwa kuanza saa 7 za mchana hadi majira ya saa 12 za jioni.
Akiongea na mwandishi wa blog hii. Rev. Eliah Mwakibete amesema kuwa nyimbo zilizomo katika album yake hii ni moto wa kuotea mbali katika kuburudisha, kuelimisha na kufikisha Injili kwa jamii husika kupitia nyimbo. aliwataja baadhi ya watakaomsindikiza katika uzinduzi huo ni pamoja na: Tully Mfaina Mbaga, Rebecca I. Magaba, Silas Mbise, Moses J. Kiyoho
Production nzima imefanywa na kampuni ya HVP Studio (Haji'z Video Production) na itakuwepo pia katika uzinduzi huu. Camera Operators: Hassan Haji Ndunda, Lusekelo George Mwamwaja na Salum Diva Sasamalo
0 Comments