ELLINAH Wamukoya ameteuliwa kuwa Askofu wa Kwanza wa
Kike wa Kanisa la Kianglikana barani Afrika. Akiongea muda mfupi baada
ya kuteuliwa, Bi. Ellinah Wamukoya amesema uamuzi huo ni heshima kwa
kina mama. Ellinah Wamukoya, 61, sasa atahudumu kama askofu mpya wa
kanisa hilo katika ufalme wa Swaziland, moja wapo ya nchi zinazokisiwa
kufuata siasa za kihafidina. Kutawazwa kwake kumejiri huku Kanisa la
Kianglikana, likitarajiwa kujadili ikiwa kina mama wataruhusiwa
kuapishwa kuwa maaskofu wa kanisa hilo.
Ellinah Wamukoya ameteuliwa kuwa askofu wa kwanza wa kike wa kanisa la Kianglikana barani Afrika.
Askofu wa jimbo la Cape Town, nchini Afrika Kusini, amesema kuwa
wamechukua uamuzi huo ili wawe mfano kwa wengine na pia kuwatakia,
viongozi wa kanisa hilo, faraja na hekima ili kujadilia suala hilo kwa
haraka. Kwa mujibu wa ripoti aliyotuma kwa vyombo vya habari, askofu
huyo wa Jimbo la Cape Town, Revd. Thabo Makgoba, amesema wimbi kwa sasa
linavuma na kuwa wameshuhudia tukio la kihistoria ambao ni sawa na mbingu
kufunguka.
David Dinkebogile aliongoza sherehe hizo na kukariri kuwa nia yao
kuwa ilikuwa kumuapisha askofu na wale sio mtu mweusi, muafrika na raia
wa Swaziland. Askofu Wamukoya ni meya wa zamani wa Mji Mkuu wa Swaziland
Manzini.
-BBC
0 Comments