Na Richard Bukos
Kajala aliyepandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam
Jumatatu iliyopita, muonekano wake kwa sasa uliwashangaza watu katika
mahakama hiyo baada ya kuonekana amenenepa sana kuliko alivyokuwa
uraiani.
Mwingine: “Dah! Hebu mcheki kwanza, yaani anazidi kuwa bomba kila
kukicha, sasa hivi amekuwa shavu dodo kuliko hata alivyokuwa uraiani!
Tusidanganyane jamani, piga ua kutakuwa na mtu anamtunza huyu hukohuko
aliko si bure. ”
MSANII wa filamu Bongo ambaye yuko nyuma ya nondo Gereza la Segerea, Dar es Salaam kwa mashitaka ya kuuza nyumba iliyowekewa kizuizi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Kajala Masanja anaweza kupata gonjwa la moyo kufuatia kunenepa sana akiwa gerezani humo.
Kajala Masanja wakati akipandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam Jumatatu iliyopita.
Kajala aliyepandishwa katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam
Jumatatu iliyopita, muonekano wake kwa sasa uliwashangaza watu katika
mahakama hiyo baada ya kuonekana amenenepa sana kuliko alivyokuwa
uraiani.
Baadhi ya watu walisikika wakihojiana wenyewe kwa wenyewe
kama kuishi gerezani kwa muda mrefu kunasababisha mtu kunenepeana kama
yeye.
“Hivi kumbe gerezani kunaweza kumnenepesha mtu jamani? Kajala
shavu dodo,” alisema mwanamke mmoja ambaye mwenzake alikuwa kinyume
naye.
Mwenzake: “Ila kunenepa kwa aina hii halafu unakaa kwa muda
mrefu kuna hatari ya kupata magonjwa ya moyo. Unajua uraiani chakula
kinachukuliwa na kazi za siku nzima, gerezani muda mwingi ni kukaa tu,
inabidi afanye mazoezi ya kupungua.”
Mwingine: “Dah! Hebu mcheki kwanza, yaani anazidi kuwa bomba kila
kukicha, sasa hivi amekuwa shavu dodo kuliko hata alivyokuwa uraiani!
Tusidanganyane jamani, piga ua kutakuwa na mtu anamtunza huyu hukohuko
aliko si bure. ”
Hata hivyo, miongoni mwa waliodatishwa na
muonekano wa Kajala ni msanii mwenzake, Mahsein Awadh ‘Dokta Cheni’
ambaye alimsogelea na kutaka kumkumbatia lakini alizuiliwa na askari
waliokuwa wakimlinda.
...akiwa na sura ya tabasamu.
0 Comments