Alma *Najma*
Najma au wengi hupenda kumuita Alma ni binti pekee katika familia ya Bwana na Bibi Abdallal Maganga aliyesoma na hivi karibuni atabahatika kupata Digrii yake ya Bachelor Degree In Social Work pale katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii *Institute of Social Work* pale Kijitonyama Dar es Salaam.
Mbali na hayo Alma ni Binti mwenye jitihada kibao za kutafuta malengo ya baadae katika maisha yake na ndio maana alijituma kwa hali na mali katika kulifikia hili lililoko mbele yake kwa sasa.
Shukrani za pekee ziwaendee wazazi wake akiwemo Mama yake Mkubwa Mrs. SS Kalembo, Mama yake mdogo Mrs Miriam Aziz, ndugu jamaa na wote walioshiriki kwa njia moja ama nyingine kumfikisha hapa alipopafikia na pia anawashukuru marafiki zake aliokuwa nao muda wote akiwa chuoni.
Mahafali yatafanyika tarehe 7 Desemba 2012 Taasisi ya ustawi wa Jamii Kijitonyama na kufuatiwa na tafrija itakayofanyika nyumbani kwao Mtaa wa Ngorongoro Chang'ombe Dar es Salaam.
|
0 Comments