Ripoti ya Shirika la Amnesty
International imefichua kuwa Wanajeshi wa Sudan Kusini wanaoendeleza
zoezi la kuwapokonya wenyeji silaha haramu mashariki mwa nchi hiyo,
wanatumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia.
Shirika hilo linasema Wanajeshi hao wanafanya vitendo vya mauaji na ubakaji.
Serikali ilizindua zoezi hilo katika juhudi za
kurudisha amani mapema mwaka huu kufuatia mapigano ya kikabila
yaliyozuka katika Jimbo la Jonglei ambako mamia ya watu waliuawa.
Hata hivyo, visa vya mateso na unyanyasaji
vimeripotiwa kutoka kwa Wanajeshi na Polisi wanaosaka Silaha haramu
zinazotumika kwenye mapigano hayo.
Mwandishi wa BBC amesema kwamba hapo awali
Serikali ilipuuza tetesi kuhusiana na visa hivyo vya mateso na
unyanyasaji tangu Taifa changa la Sudan Kusini lilipojinyakulia uhuru
wake zaidi ya mwaka mmoja uliopita
0 Comments