Mikutano ya Vuguvugu la Mabadiliko
(M4C) inayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
wilayani hapa, Mkoa wa Geita, imezoa makada 201wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), akiwamo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Buhungu, Kata ya Kigongo.
Makada waliotimkia Chadema kutoka Jimbo la Chato linalowakilishwa na
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa nyakati tofauti, wanatoka
katika Kijiji cha Muganza, Kasenga, Busaka na Igando, Kata ya Bwera,
ambako chama hicho kimefanya mikutano ya hadhara.
WanaCCM hao walidai wamekihama chama hicho kwa sababu wamechoshwa na
mwenendo wa siasa zake, walizodai zimechangia maisha ya wananchi kuwa
magumu.
0 Comments