Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akiuaga mwili wa Marehemu Liberatus Barlow
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo Marehemu Liberatus Barlow
Mwili
wa marehemu Kamanda Barlow ukimwagiwa maji ya baraka na Paroko wa
Kanisa la Nyakahoja, Padre, Raymond Manyanga (hayupo pichani) katika
ibada ya kumuombea marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Dar es
Salaam.
Umati ukiwa katika viwanja vya Nyamagana kumuaga Kamanda Marehemu Liberatus Barlow
Familia ya marehemu Kamanda Barlow ikiwa katika majonzi (Picha zote na http://gsengo.blogspot.com/)
MWILI wa aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa
wa Mwanza, Marehemu Liberatus Barlow umeagwa katika Uwanja vya Michezo
wa Nyamagana, ambapo viongozi wa kada mbalimbali na wananchi kutoka
wilaya zote za mkoa wa Mwanza na mikoa jirani wametoa heshima za mwisho
kwa marehemu Kamanda huyo wa Polisi.
Baada ya kuagwa na viongozi mbalimbali na wananchi, mwili wa marehemu
Kamanda Barlow umepelekwa kwa msafara katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza,
ambapo utasafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam nyumbani kwake.
Taarifa zinafafanua baada ya kufikishwa Dar, maofisa wa Jeshi la
Polisi Makao Makuu jijini Dar es Salaam, ndugu, jamaa, marafiki na
wananchi watatoa heshima za mwisho kwa marehemu Kamanda Barlow, kisha
mwili utasafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro, Marangu kwa mazishi.
Miongoni mwa viongozi mashughuli walioshiriki kuuaga mwili wa kamanda
huyo leo mjini mwanza ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,
Evarist Ndikilo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI),
Robert Manumba, Lawrance Masha ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Taifa CCM, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Geita, Joseph Kasheku, Mbunge wa
Rolya Lameck Airo na wabunge wengine. Pia wamehudhuria makamanda wa
Jeshi la Wananchi na Maofisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi, pamoja na
wafanyabiashara anuai.
0 Comments