Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU),
wakimkamata mmoja wa wafuasi wa kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za
Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda, wakati kikundi cha wafuasi hao
kilipojaribu kuandamana kuelekea Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es
Salaam, kwa lengo la kushinikiza kiongozi huyo aachiwe. Ponda alitiwa
mbaroni kwa mahojiano kuhusiana na ghasia za wiki iliyopita eneo la
Mbagala ambako makanisa kadhaa yalichomwa moto.
Na Mwandishi wetu
0 Comments