Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk. Mohammed Shein
Breaking Newzzzz Zanzibar!
Taarifa ambazo mtandao wa Thehabari.com umezipata
muda huu ni kwamba; Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk.
Mohammed Shein amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri kwa
kuwaondoa baadhi na kuteua wengine.
Katika mabadiliko hayo Dk. Shein amemuondoa Waziri asiyekuwa na
Wizara Maalum, ambaye ni mjumbe wa baraza hilo, Mansoul Yusuf Himid na
nafasi yake kumteuwa waziri mwingine kushika nafasi hiyo, Shaur Buheti
Hassan. Dk. Shein amefanya mabadiliko kwa manaibu mawaziri ambapo
amemteuwa Mtumwa Mbarak kuwa Nabu Waziri Wizara ya Kilimo na Maliasili
na Mohamed Said Mohamed kuwa Naibu Waziri Wizara ya Kilimo na Uvuvi.
Hata hivyo taarifa zinasema Dk. Shein amefanya mabadiliko kwa
makatibu wakuu, ambapo amemteuwa Dk. Juma Akil kuwa Katibu Mkuu Wizara
ya Miundombinu na Mawasilio na Mustafa Abood Juma kapewa wizara ya Ardhi
Zanzibar.
Taarifa zaidi juu ya mabadiliko haya tutawaletea kesho katika habari
mara baada ya kuipata kwa kina. Endelea kufuatilia mtandao wako kwa
taarifa za uhakika.
0 Comments