Raia wawili wa Kenya wamefariki dunia
papo hapo na wengine watatu wamejeruhiwa vibaya baada ya magari mawili
waliyokuwa wakisafiria aina ya Canter kuligoga basi la abiria mali ya
kampuni ya Super Feo lililokuwa likitoka Songea kuelekea Dar es Salaam.
Habari zilizopatikana mjini Songea mkoani Ruvuma zimedai kuwa ajali hiyo
ilitokea jana majira ya saa 3:00 asubuhi katika kijiji cha Wino
wilayani Songea karibu na mpaka wa Mkoa wa Ruvuma na Njombe na watu
wawili waliokuwa kwenye Canter ambao ni dereva na utingo wake walifariki
dunia papo hapo baada ya gari hilo kugongana na basi hilo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, majeruhi watatu ambao walikuwa ni
abiria wa basi la Super Feo ambao majina yao hayakuweza kupatikana mara
moja walikimbizwa katika Hospitali ya Serikali ya Wilaya ya Njombe kwa
matibabu zaidi huku miili ya marehemu wawili wa ajali hiyo ikihifadhiwa
katika kituo cha afya cha Madaba wilayani Songea.
Walieleza kuwa Canetr iliyokuwa imesheni nyama ya kuku pamoja na mayai
ilikitokea wilayani Mufindi, mkoani Iringa ikiwa kwenye mwendo kasii
kwenye na iligongana na basi hilo ambalo lilikuwa likitoka Songea
kuelekea Dar es Salaam na baadaye basi hilo liliendelea na safari.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Deusdedit Nsimeki, alithibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kusababisha vifo raia hao wa Kenya na
majeruhi watatu.
0 Comments