Ajali Mbaya Yatokea Mbeya Yauwa 10 na Kujeruhi 25


Gari ambalo alikuwemo Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mary Mwanjelwa likiwa limeteketea kwa moto baada ya ajali.


  Baadhi ya magari yaliohusika katika ajali hiyo yakiwa yameharibika vibaya


Lori la mafuta lililosababisha ajali hiyo likiendelea kuteketea kwa moto huku wananchi wakishuhudia muda mfupi baada ya ajali hiyo.


Mbunge Mary Mwanjelwa akiwa amelazwa hospitalini baada ya kuokolewa kwenye ajali hiyo.


WATU kumi wamekufa na wengine 25 kujeruhiwa akiwemo Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Mary Mwanjelwa baada ya lori la mafuta kushindwa kushika breki na kuyagonga magari mengine matatu katika mtelemko wa Mlima wa Iwambi eneo la Mbalizi nje kidogo ya Jiji la Mbeya.

 

Katika ajali hiyoiliyotokea majira ya saa nane mchana, Mbunge Mwanjelwa alinusurika kufa baada ya gari alilokuwa akisafiria, kugongwa na kuteketea kwa moto kabisa na kusababisha kifo cha Katibu wake. Mbunge huyo kwa sasa amelazwa katika Hospitali Teule ya Ifisi kwa matibabu zaidi pamoja na majeruhi wengine.

 

Baadhi ya watu waliioshuhudia ajali hiyo, walisema lori hilo la mafuta lilishindwa kushika breki na kuanza kutelemka kwa kasi katika mlima huo, ambapo liliyagonga magari matatu ikiwamo gari dogo la abiria (Hiace) yenye namba za usajili T 587 AHT na kuleta madhara zaidi.

 

Kwa upande wake, Muuguzi wa Hospitali ya Ifisi, Sikitu Mbilinyi alisema Mbunge Mwanjelwa analalamika zaidi maumivu katika sehemu ya mgongoni na miguu sawa na dereva wake ambaye naye analalamikia miguu na amepasuka sehemu ya kichwani. Majeruhi wengine wengi wamekatika miguu kutokana na kitendo cha lori hilo kugonga gari aina ya hiace ubavuni kabla ya kuanguka.

 

 LIVE!HIVI NDIVYO MUHESHIMIWA MBUNGE WA VITI MAALUM MARY MWANJELWA PAMOJA NA DEREVA WAKE WALIVYO SAFIRISHWA KUELEKEA DAR ES SALAAM KWA MATIBABU ZAIDI!

 MKE WA DEREVA WA MBUNGE ALIYE VAA KHANGA NYEKUNDU WAKIWA PAMOJA NA DR. MAMA KANAMA
 DEREVA MH.MBUNGE AKIWA ANAINGIZWA NDANI YA NDEGE SASA
 MH. MBUNGE HILDA NGOYE AKIMUAGA DEREVA WA MH.MARY MWANJELWA 
 DR.NZUNDA WA MBELE AKIWA ANAMPELEKA MUHESHIMIWA MBUNGE KUPANDA NDEGE
 MUHESHIMIWA MBUNGE, MARY MWANJELWA AKIWA ANAPANDISHWA KATIKA NDEGE 
 HII NDIO NDEGE AMBAYO MUDA SI MREFU ITARUKA KUELEKEA DAR ES SALAAM 
MUHESHIMIWA MKUU WA MKOA ABASS KANDORO AKIWA ANAAGANA NA MH.MBUNGE WA VITI MAALUM MARY MWANJELWA 
 MH. MKUU WA WILAYA WA MBEYA AKIWA ANAMUAGA MH MBUNGE
 SHUGHULI YA KUAGA INAENDELEA 
 VIONGOZI MBALIMBALI WA CHAMA NA SERIKALI 
 NDEGE HIYO INAONDOKA SASA
 WATU MBALIMBALI WAKIPUNGA MKONO WA KWAHELI NA ISHARA YA UPENDO KWA MARA BAADA YA NDEGE KUONDOKA
NDEGE NDIYO HIYO INAKARIBIA KUPAA... KUELEKEA DAR ES SALAAM

*

Post a Comment

0 Comments