Waziri wa Serikali za Mitaa nchini Kenya, Fred Gumo
WAZIRI mmoja wa Kenya amekanusha kuwa anahusika na
wizi wa gari moja la wizi ambalo amekutwa nalo. Waziri hiyo ambaye ni wa
Serikali za Mitaa nchini Kenya, Fred Gumo, alisema gari lake alikuwa
amempa mfanyabiashara mmoja wa Mombasa na badala yake akakabidhiwa gari
hilo ambalo ni la wizi bila kujua, ambalo lilikuwa limeibwa kutoka kwa
rais wa zamani, Daniel Arap Moi, miaka mine iliyopita.
Bwana Gumo amesisitiza kwamba hakujua kuwa gari hilo lilikuwa la
kuibiwa. Hata hivyo alisema hakulitumia sana gari hilo kwa sababu
hakupata nyaraka zote za gari hilo.
0 Comments