Baadhi
ya waumini wa dhehebu la Kiislamu wakiandamana ikiwa ni hatua ya
kulaani filamu iliyotengenezwa nchini Marekani ya kumkashfu Mtume
(S..A.W)
Waumini
wanawake wa dini ya Kiislamu wakiandamana jijini Dar es Salaam eneo la
Kidongo Chekundu kulaani filamu ya kumkashfu Mtume wao iliyotengenezwa
nchini Marekani
Mmoja wa waandamanaji akizungumza na vyombo vya habari kuelezea nia ya maandamano yao
Baadhi
ya waumini wa dhehebu la Kiislamu wakiandamana ndani ya Uwanja wa
Kidongo Chekundu Dar es Salaam ikiwa ni hatua ya kulaani filamu
iliyotengenezwa nchini Marekani ya kumkashfu Mtume (S.A.W).
BAADHI ya waumini wa dini ya Kiislamu leo jijini Dar es Salaam wamefanya maandamano katika viwanja wa Kidongo Chekundu ikiwa ni hatua ya kuungana na Waislamu katika nchi mbalimbali kupinga filamu iliyotengenezwa nchini Marekani ikimkashfu kiongozi wao (Mtume) pamoja na dini ya Kiislamu.
Maandamano hayo yalianza majira ya mchana mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa kwa misikiti mbalimbali hasa ile ya kati kati ya jiji, ambapo waumini waliongozana kuelekea katika Viwanja vya Kidongo Chekundi vilivyopo pembezoni mwa eneo la Mnazi Mmoja.
Taarifa za awali zilieleza awali waumini hao kupitia viongozi wao waliomba kibali cha kufanya maandamano kuelekea viwanja vya Jangwani lakini walizuiwa kutokana na uwanja huo kuwa na shughuli zingine. Baada ya kuzuiwa waliamua kuandamana kwenye eneo hilo bila kibali chochote lakini hakukuwa na kikwazo chochote.
Waandamanaji walionekana wameshika mabango yaliokuwa na ujumbe wa kuyalaani mataifa ya Marekani na Israel huku wakiitaka Serikali kufuta ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kutokana na filamu wanayoilalamikia kutengenezwa katika taifa hilo.
Vikosi vya FFU vikiwa tayari kupambana na waandamanaji endapo watavuka viwanja vya Kidongo Chekundu

0 Comments