
Treni
ya Reli ya Kati ikipita katika eneo la Tabata ilipokuwa katika
majaribio ya kubeba abiria wa jijini Dar es Salaam kwa kufanya safari
kuanzia Stesheni mpaka Ubungo na kurudi Stesheni. Treni hiyo inatalajiwa
kuanza rasmi huduma hiyo mwezi ujao. Picha na Edwin Mjwahuzi
Mwandishi wetu
Usafiri wa treni jijini Dar es saklaam utaanza mwezi
Oktoba baada ya kukamilika kwa maboresho ya reli kutoka Ubungo hadi
stesheni.
Akizungumza jana baada ya kufanya safari ya majaribio
Naibu waziri wa Dk Charles Tizeba alisema kufikia mwezi ujao treni hyo
ityaanza kubeba abiria ili kupunguza matatizo ya usafiri kwa wakazi
waishio maeneo inapopita treni hiyo.
“Kufika Oktoba tutakuwa tumeanza
kutoa huduma maana leo tumeanagalia uwezekano na tumeona tunaweza
ufanya huduma na kurekebisha kasoro zilizobaki” alisema Dk Tizeba .
Dk
Tizeba alisema kuwa reli hiyo kwa sasa bado haijakaa vizuri hivyo
inahitaji kurekebishw aili trenio hiyo iwee kwenda kasi zaidi na
kubomolewa kw anyumba zilizojengwa jirani na reli hiyo.
“Inashangaza
sana kwani kuna watu wamejenga nyumba zao jirani kabisa na reli na
wengine wamediliki kujenga mita moja kutoka relini, hii inahatarisha
maisha yao wengyewe na hata wasafiri watakaotumia ttreni”
Hivyo
alisema kuwa tayari watu hao wametaarifiwa juu ya kuondoka katika maeneo
hayo na kwamba watatakiwa kuvunja wenyewe na wakikaidi basi watavunjiwa
ili huduma hiyo ianze kutolewa.
0 Comments