Baadhi ya Mashabiki wakiwa wamefurika katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Mkoa wa Mbeya ndani ya Uwanja wa Sokoine
Wasanii wa Filamu hapa nchini Aunt Ezekiel, Wema pamoja na Shilole wakiwasikiliza mashabiki wao wanataka nini.
Msanii
mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Diamond akiwaimbisha mashabiki na
wapenzi wa muziki huo waliojitokeza kwa wingi usiku huu kwenye tamasha
la Serengeti Fiesta, kwenye uwanja wa Sokoine, mkoani Mbeya.
Shemejiii….Wema Sepetu akiwachetua kidogo wapenzi wa mambo ya filamu.
Msanii wa
bongofleva kutoka THT, Barnaba akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu
kwenye tamasha la serengeti fiesta 2012 ndani ya uwanja wa Sokoine
mkoani Mbeya.
Wadau wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea usiku huu.
Watu kibao ndani ya sokoine usiku huu.
Mmoja
wa wasanii mahiri wanaotikiza kwenye anga ya muziki wa Bongofleva hasa
katika miondoko ya R&B, Ben Paul akikamua vilivyo jukwaani huku
mashabikiwa wake wakishangilia kwa shangwe.
Pichani
kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dk. Norman Sigallah akimtaja mshindi
wa gari aina ya Vits itolewayo na kampuni ya Push Mobile, ikiwa ni
sehemu mojawapo ya mchakato wa Tamasha la Serengeti Fiesta 2012,
anayeshuhudia ni Meneja Masoko wa Push Mobile, Rugambo Rodney na kulia
ni Chiku Saleh kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha, ambapo katika
bahati nasibu hiyo iliyochezeshwa, aliyeibuka mshindi ni Eva B
Mgovani.
ni full kujiachi tuu ndani ya uwanja wa sokoine usiku huu.
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya anaefananishwa na mashabiki wake kama Ray C,
aitwaye Recho kutoka THT akitumbuiza jukwaani usiku huu ndani ya tamasha
la Serengeti Fiesta 2012
Mashabiki wakishangilia vilivyo usiku huu, huku makamuzi ya wasanii yakiendelea jukwaani.
Msanii
wa bongofleva anaetikisa kwa nyimbo kadhaa ikiwemo, Mama halima, Aifora
na nyinginezo akiwaimbisha mashabiki wake kama waonekanavyo pichani
usiku huu.
Mkali
mwingine anaekuha juu katika mambo ya kuchana a.k.a kughani Stamina
akiamsha kitim kitim kwa wakazi wa mji wa Mbeya usiku huu ndani ya
tamasha la Serengeti Fiesta.
0 Comments