R.I.P. MZEE JOSEPH PETER BABILE

R.I.P. MZEE BABILE

Marehemu Joseph Peter J. Babile

MAREHEMU JOSEPH PETER J. BABILE

Alizaliwa tarehe 19 Machi' 1953 katika Manispaa ya Sumbawanga, mnamo mwaka 1960 alijiunga na elimu ya msingi katika shule ya Seminari Kantalamba na kuhitimu darasa la saba mwaka 1967. Mwaka 1968 alijiunga na elimu ya Sekondari katika Seminari ya Kaengesa na kuhitimu kidayo cha nne mwaka 1972, mwaka 1974 alijiunga na kozi ya Ualimu katika Chuo cha Ualimu Morogoro na kuhitimu mwaka 1976 ambapo alitunukiwa cheti cha Ualimu daraja "A".


Baada ya kumaliza mafunzo ya ualimu Marehemu Babile aliajiriwa na Wizara ya Elimu akiwa Mwalimu na kufundisha katika shule mbali mbali zikiwemo shule za Sekondari Milambo na Uyui zilizoko Tabora. Mnamo mwaka 1981 alifanya mitihani ya kidato cha sita katika kituo cha Milambo Sekondari akiwa mtahiniwa binafsi na kufanikiwa kufaulu mitihani hiyo. Mwaka 1982 Marehemu alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya shahada ya kwanza na kuhitimu mwaka 1985.

Marehemu Joseph Babile (wa kwanza kushoto) na (katikati) ni Mkuu wa Chuo Dk. Magoti

Marehemu Joseph Peter Babile aliajiriwa na kilichokuwa Chuo cha Chama Kivukoni na kupangiwa Chuo cha Chama kanda ya Lushoto akiwa Mwalimu kuanzia tarehe 01 Oktoba' 1988. Mwaka 1992 marehemu alihamishiwa Chuo cha Chama Kivukoni na mwaka huo huo alirithiwa na kilichokuwa Chuo cha Sayansi Jamii Kivukoni.


Mwaka 1993 marehemu alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa masomo ya Shahada ya Uzamili katika taaluma za maendeleo na kuhitimu mwaka 1996


Tarehe 01 Oktoba' 2005 marehemu Babile alirithiwa na Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere akiwa Mhadhiri


Mwaka 2011 marehemu Babile alianza kusumbuliwa na maradhi ya mguu ambapo alitibiwa katika Hospitali mbalimbali zikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mikocheni Mission Hospital na Ocean Road. Marehemu Joseph Peter Babile amefariki tarehe 31 Agosti' 2012 na kuzikwa tarehe 03 septemba' 2012 katika makaburi ya Kisiwani Vijibweni Kigamboni Dar es Salaam.


Marehemu Babile katika uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali Chuoni, nyadhifa hizo ni Mshauri wa Wanafunzi, Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi - RAAWU (Tawi) na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya RAAWU Kanda ya Mashariki


Marehemu Joseph Peter Babile amecha Mjane, Watoto na Wajukuu na tutazidi kumkumbuka milele, Mungu ailaze roho ya marehemu Babile mahali pema peponi - amen

Ona matukio ya Picha hapa chini:

Mke wa Marehemu Babile (kulia) katika majonzi

Mwakilishi toka MNMA na MC Mr. Grayson Mwikola



Mr. Kazeze Mwenyekiti Baraza la Walei Parokia ya Kigamboni ya Mt. Maria Konsolata

Rais wa MASO MNMA akitoa rambirambi kwa mke wa Marehemu


Wanafunzi ambao walihitimu Chuo cha Kumbukumbu wa Mwl. Nyerere miaka ya nyuma walishiriki pia na kutoa rambirambi yao na masikitiko yao kuhusu kifo cha Mhadhiri Joseph Babile


Mwakilishi toka Ofisi ya Rais Mipango anakofanyakazi mmoja wa watoto wa marehemu akikabidhi rambirambi kwa Mke wa Marehemu


Waombolezaji wakipita kuuaga mwili wa marehemu Babile


Diwani wa Kitongoji cha Tungi Mzee Luambano aliuaga mwili wa marehemu Babile









Post a Comment

0 Comments