Hassan Sheikh Mohamud Somalias
RAIS mpya wa nchi ya Somalia Hassan Sheikh Mohamud,
amenusurika jaribio la kumuua mjini Mogadishu. Milipuko miwili imetokea
nje la lango la makao ya rais huyo katika hoteli ya Al-Jazeera wakati
rais huyo alipokuwa anajiandaa kufanya mkutano na waandishi wa habari.
Taarifa zinasema kuwa waziri wa mambo ya nje wa Kenya Sam Ongeri pia
alikuwa katika hoteli hiyo wakati wa shambulizi. Hata hivyo wawili hao
wamenusurika. Inaarifiwa watu wanne wameuawa na wengine watatu
kujeruhiwa.
Balozi wa Marekani auawa Libya
BALOZI wa Marekani nchini Libya ameuawa baada ya
kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami na kuvamia ubalozi wa Marekani
Mashariki mwa mji wa Benghazi. Balozi Christopher Stevens, ni miongoni
mwa maafisa wengine wa ubalozi waliouawa kufuatia maandamano kuhusu
filamu iliyotolewa nchini humo ikimkejeli Mtume Muhammad.
Idara ya mambo ya ndani nchini Marekani, imethibitisha tu kifo cha
afisaa mmoja wa ubalozi huo ingawa bado haijataja jina lake. Maandamano
ya kupinga filamu hiyo pia yalifanyika mjini Cairo dhidi ya ubalozi wa
Marekani.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton, amelaani mashambulizi hayo.
Serikali ya Libya imetaja shambulio hilo kama kitendo cha uoga. Ubalozi
huo uliteketezwa na watu waliojihami kwa bunduki kulalamikia filamu moja
iliyotengenezewa nchini Marekani ambayo wanasema inamdhihaki Mtume
Mohammed.
Wanamgambo hao wanaoripotiwa kuwa na ufungamano na kundi la waislamu
wenye msimamo mkali walitumia maguruneti ya kurushwa kwa roketi kuvamia
ubalozi huo kabla ya kuiteketeza. Maafisa wa Libya wameiambia BBC kwamba
hali imetulia kwa sasa.
Machafuko hayo ya Libya yalijiri saa kadhaa baada ya maelfu ya
waandamanaji kukusanyika nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kuelezea
hasira zao kuhusu filamu hiyo kumhusu Mtume Mohammed. Kwa wakati mmoja
waandamanaji hao waliingia ndani ya ubalozi huo na kuichana bendera ya
Marekani na kurejesha yao.
0 Comments