
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Said Mwema
Na Mwandishi Wetu, Arusha
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha limezuia mwaandamano ya amani ya
waandishi wa habari mkoani hapa yaliopangwa kufanyika kwa nia ya
kulaani mauaji ya mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten, Daudi
Mwangosi.
Taarifa ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Arusha (OCD), Lotson Mponjoli,
yenye namba AR/B. 5/VOL. II/75 kwa uongozi wa Chama Cha Waandishi Mkoa
wa Arusha (APC), imesema wamezuia maandamano hayo kwa madai kupisha
shughuli za kiserikali zinazoendelea mjini hapa.
“Napenda kuwajulisha kwamba ni vema mkasitisha maandamano yenu
mliyoazimia kuyafanya, kwa kuwa wiki hii yote tutakuwa na shughuli za
kiserikali kwani tutakuwa na ugeni mkubwa wa uongozi we Serikali
kimataifa wanaohudhuria mkutano wa mazingira,”
“Pia tuna maandalizi ya mtihani wa darasa la saba, hivyo hakutakuwa
na askari wa kutosha katika kulinda na kuongoza maandamano,” alisema na
kuongeza katika taarifa hiyo. Alidai kuwa kutoka na serikali kuchukulia
suala hilo la mauaji kwa uzito wake, hivyo wanahabari tuwe na subira kwa
matokeo kwani Serikali kupitia tume iliyoundwa itatoa taarifa juu ya
jambo hilo.
Awali Jeshi la Polisi lilizuia maandamano hayo ambayo yalipangwa
kuanzia eneo yalipo Makao Makuu ya CCM, ambapo kabla ya kufika kwa
polisi hao kundi kubwa la wanahabari wakiwa na mabango yenye ujumbe
mbalimbali ya kulaani mauaji hayo. Aidha baadhi ya wanahabari walipinga
vikali kitendo cha polisi kuzuia maandamano hayo kwa madai kwamba kuna
uhaba mkubwa wa polisi wa kulinda maandamano, huku ikidaiwa pia kwa
sababu ya ugeni mkubwa wa mkutano wa mazingira unaoendelea.
Walidai kuwa jeshi hilo halikupaswa kuzuia maandamani hayo kwani
wajibu wao ni kupewa taarifa na kulinfa maandamano, ambapo pia walidai
kuwa hawahitaji Polisi kuwalinda. Kwa upande wake Katibu wa (APC) Eliya
Mbonea, akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wengine wa chama hicho
walifika katika eneo hilo na kuwaomba wanahabari kutii amri hiyo
iliyotolewa na Polisi.
Baada ya maelezo hayo, waandishi walilazimika kusitisha maandamano na
kuondoka katika eneo hilo huu kukiwa na gari la polisi waliokuwa
wakiongozwa na OCD, katika eneo hilo ambao nao waliondoka baada ya
kusitishwa kwa maandamano hayo.
0 Comments