KILA MMOJA AJITWISHA JUKUMU LA KUWASOMESHA, WAPIGANA VIJEMBE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2015
Hawa Mathias, Mbeya na Tumaini Msowoya, Iringa
MAZISHI ya Mwandishi wa Habari, Daud Mwangosi yalifanyika jana katika Kijiji cha Busoka kilichoko wilayani Rungwe, Mbeya na kuhudhuriwa na mamia ya waombolezaji wakiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa. Katika mazishi hayo, viongozi hao wawili kila mmoja alitangaza kuwasomesha watoto wa marehemu Mwangosi ambaye alifariki dunia Septemba 2, mwaka huu baada ya kupigwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu wakati polisi walipokuwa wakisambaratisha mkutano wa Chadema.
Akitoa salamu
zake katika mazishi hayo, Profesa Mwandosya alisema yupo tayari
kumsomesha mtoto wa kwanza kati ya wanne wa Mwangosi, Nehemia ambaye
anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Malangali.
Alisema atamsomesha mtoto huyo kidato cha tano na sita na ikiwa atafaulu na kukosa mkopo wa elimu ya juu, atamsomesha mpaka atakapomaliza elimu yake ya juu.
Dk Slaa kwa upande wake, alisema amewasiliana na rafiki
yake ambaye yupo tayari kuwasomesha watoto wawili wa Mwangosi ambao wote
wapo shule ya msingi. Mtoto wa mwisho wa marehemu hajaanza masomo.
Pamoja na kuwasomesha watoto hao, alisema Chadema kimetoa Sh2 milioni za rambirambi kutokana na msiba huo.
Vijembe msibani
Awali, Profesa Mwandosya na Dk Slaa walitoa kauli zinazoonyesha kupigana vijembe vya kisiasa, baada ya waziri huyo kumtaka Dk Slaa aache kufanya kampeni za kuingia Ikulu mwaka 2015 msibani.
Kauli hiyo ya Profesa Mwandosya ilikuja baada ya Dk Slaa kutaka polisi waliohusika na mauaji hayo wachukuliwe hatua za kisheria kwa sababu wanajulikana.
“Tunashangaa
wamekamatwa watu wengine na kuwaacha waliohusika na mauaji hayo,
tunawajua kwa sababu wameonekana hadharani, hakuna siri kwa hilo,”
alisema Dk Slaa.
Akizungumza baada ya kauli hiyo ya Dk Slaa,
Profesa Mwandosya aliwataka wanasiasa wa vyama vya upinzani kuacha
kutumia misiba kutafuta kura za urais mwaka 2015.
“Natoa pole
sana kwa familia na tasnia nzima ya habari nchini. Hiki ni kipindi
kigumu, lakini tuviachie vyombo husika vifanye uchunguzi wa mauaji
haya,” alisema Profesa Mwandosya na kuongeza:
“Lakini nichukue fursa hii kuwaomba wanasiasa waache kutumia misiba ili kujipatia umaarufu katika kutafuta kura za urais mwaka 2015.”
Katika mahubiri yake
msibani hapo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT), Busoka, Mathayo Mwanjemele alikemea mauaji hayo na kuwaomba
wahusika wajitokeze hadharani kabla Mungu hajawaumbua.
“Waliohusika na mauaji haya wajitokeze na kutubu kwa wananchi kabla adhabu ya Mungu haijawakuta,” alisema.
Alisema ufike wakati Serikali iwe inakiri uzembe unaofanywa na watendaji wake ambao umekuwa ukitokea mara kadhaa.
IGP Mwema asimamia uchunguzi
Kabla
ya mazishi hayo, mwili wa Mwangosi ulifanyiwa uchunguzi na wataalamu wa
afya kutoka Dar es Salaam, huku IGP Said Mwema akishuhudia.
Baada ya kumalizika uchunguzi huo, usiku mwili wa marehemu ulisafirishwa kuelekea Mbeya kwa mazishi.
Mwili huo ulipofika Tukuyu, umati mkubwa ulijipanga barabarani na kupunga mkono, huku wengine wakiusindikiza kwa baiskeli na pikipiki hadi kijijini, Busoka.
Majeruhi wengine
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mafinga, Dk Peter Mwenda alisema mbali na marehemu Mwangosi, watu wengine 10 walijeruhiwa, wawili kati yao walitibiwa na kuruhusiwa. Alisema waliobaki hospitalini hapo hali zao zinaendelea vizuri.
Aliwataja majeruhi hao kuwa ni Hussein Kweha
(27), Edson Iddy (22), Alfred Kibitanyi (27), Hamad Musa (37), Yeremia
Kulwa (45) na Christopher Pesa (30).
Alisema majeruhi hao walidai
kwamba walikuwa katika mkutano wa ndani wa Chadema na askari waliwataka
kutulia kabla ya kuwashambulia kwa marungu na vitu vyenye ncha kali.
Pata habari na picha zaidi: kwa hisani ya Mbeyayetu.blogspot.com
UPDATES!! TUKIO ZIMA LA MAZISHI(SAFARI YA MWISHO) LA MPIGANAJI MWANDISHI WA CHANEL TEN DAUDI MWANGOSI, TUKUYU MBEYA.
Waandishi wa Habari wakiwa wamebeba Mwili wa Marehemu kuelekea Makaburini
Wakiwa wanafanya ibada ya Mwisho kabla ya kuanza maziko
Hapa wakiwa wanashusha mwili wa marehemu katika Nyumba yake ya milele
Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi ukiwa Tayari katika Kaburi
Shughuli za kuzika zimeanza
Mazishi yanaendelea
Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akiweka Shada la Mauwa kwa machungu
Mke wa Daudi Mwangosi akiwa analia kwa uchungu katika Kaburi la Marehemu Mumewe
Watoto wa Marehemu wakiwawanaweka mashada ya maua sasa
Ni ngumu sana Kuamini kwa mke wa Marehemu lakini hali ndivyo ilivyo kuwa akiwa na huzuni kubwa
Dr Slaa akiweka Shada la Mauwa
Dr Slaa Baada ya kumaliza kutoa heshima za mwisho
Mh. Mark Mwandosya akiweka Taji la maua pamoja na mke wake
Rais wa UTPC akiweka shada la Maua
Ndugu wa Marehemu akiweka shada la Maua
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akiweka shada la maua
Ndugu wa Marehemu akiweka shada la Maua
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akiweka shada la maua
Mwandishi Mkuu wa Mbeya yetu, Ndugu Joseph Mwaisango akiwa anatoa heshima zake za Mwisho katika Kaburi
Wananchi wakiwa wanarejea baada ya mazishi
Waandishi wa Habari wakichukua Tukio Live `
Na
huu Ndio Mwisho wa tukio zima la Mazishi ya Ndugu yetu, Mwanaharakati,
Mpiganaji Daudi Mwangosi aliyekuwa Mwandishi wa Chanel 10.
Mpiga picha Mkuu
alikuwa ni Ndugu Joseph Mwaisango
Updates! Hivi ndivyo zilivyo kuwa shughuli nzima za kuuaga Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi Itete Tukuyu Mkoani Mbeya
Mwili wa Marehemu Daudi Mwangosi ukiwa una andaliwa kwa ajili ya kutolewa Heshima za mwisho
Mheshimiwa Mark Mwandosya akitoa Heshima za Mwisho
Muheshimiwa Dr Slaa akitoa Heshima za mwisho
Ndugu jamaa na Marafiki wakitoa Heshima za Mwisho
Mke wa Marehemu akitoa heshima zake za Mwisho
Ma elfu ya watu wakipita kutoa Heshima zao za mwisho
Huko Jikoni Mambo yanaendelea
Mama Mzazi wa Marehemu Daudi Mwangosi akiwa analia kwa Uchungu
Dr Slaa akiwa pamoja na Mh. Mark Mwandosya
Live! Salam pamoja na Ibada ya Mazishi imeanza sasa Itete Tukuyu mkoani Mbeya katika mazishi ya Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi
Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi akilia kwa Uchungu Muda huu
Maelfu ya watu wakiongezeka kuja katika Mazishi ya mwandishi wa habari wa Chanel 10 Daudi Mwangosi Muda huu
Mheshimiwa Mark Mwandosya ambaye ni Waziri ofisi ya Rais na pia Mbunge wa Rungwe Mashariki akitoa salam kwa Niaba ya Serikali
Watu wakiwa wengi na wenye utulivu wakisikiliaza watu mbalimbali wakitoa salam zao kwa ndugu wa Marehemu
Mjane Mke wa Marehemu Daudi Mwangosi aliye jishika, akiwa na uchungu muda huu
Ibada ikiwa inakaribia kuanza
Ibada ya mazishi ndio imeanza muda huu
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa wenye majonzi Makubwa
Waandishi
wa Habari wakiwa katika msiba wa kwanza kutoka kulia ni Ndugu Joseph
Mwaisango ambaye ni mwandishi mkuu wa Mbeya yetu Blog, Rais wa UTPC Keny
Simabaya, pamoja na Felix Mwakyembe .
Liveee!! Tukio Mazishi ya Mwandishi wa Habari wa Chanel 10 Daudi Mwangosi kijijini Kwao Itete Tukuyu Mkoani Mbeya
Wawakilishi Mbalimbali wakitoa salam za Pole kwa ndugu wa Marehemu
Mwakilishi wa Chanel Ten Hamis akitoa pole katika msiba huu muda huu
Mwenyekiti wa Mbeya Press Club akitoa pole zake kwa wafiwa
Mwanaharakati Francis Godwin akielezea Jinsi Mauti yalivyo mkuta Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi
Rais
wa UTPC Kenny Simbaya ambaye pia ni kiongozi wa msafala wa kuleta Mwili
wa Marehemu Daudi Mwangosi akiwa anatoa salam za Pole kwa wafiwa.
Dr Slaa akitoa pole kwa wafiwa wote Muda huu
Wakina mama wakiwa wenye majonzi makubwa sana na huzuni muda huu
picha zote kwa hisani ya mbeyayetu.blogspot.com
Tunawashukuru sana uongozi mzima wa mbeyayetu.blogspot.com
kwa kutupatia matukio haya live. HVP Studio tunawapongeza kwa kazi nzuri na ngumu uliyoifanya
0 Comments