SERIKALI ya Malawi imeomba kuahirishwa kwa mkutano wa
wajumbe wanaoshiriki katika kutafuta muafaka wa mgogoro wa mpaka
uliotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam kesho uahirishwe.
Katika
ombi hilo, ilieleza kwamba sababu kubwa ni kwamba hatua ya awali ya
kuwakutanisha Wanasheria Wakuu wa nchi hizo mbili kubadilishana nyaraka
muhimu ambazo Serikali zitazitumia katika kutafuta suluhu hiyo.
Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi, Quent Kalichero alisema jana
kwamba wakati wa mkutano wa wajumbe hao uliofanyika Lilongwe, Malawi
wiki mbili zilizopita walikubaliana kwamba Wanasheria Wakuu wan chi zote
mbili wanatakiwa kukaa pamoja na kubadilishana uelewa wa kisheria wa
mkataba wa Anglo Germany wa mwaka 1890, hasa ibara ya 1(ii) na sehemu ya
(iv) ya mkataba wa Heligoland.
Alisema mkataba wa Anglo Germany
wa mwaka 1890 yalitiwa saini na Uingereza na Ujerumani ambao walikuwa
wakoloni wa nchi hizo mbili wakionyesha kwamba mpaka upo katika kingo za
ziwa Nyasa kwa upande wa Tanzania, lakini hili limepuuzwa.
Katika
mahojiano yake Alhamisi wiki hii, Kalichero alisema Wizara yake
imeandika barua maalum kwa wenzao wa Tanzania wakiwataka waahirishe
mkutano huo kwa kuwa Wanasheria hao wakuu wa nchi hizo hawajatimiza
wajibu wao kwa wakati.
0 Comments