MAANDALIZI YA HARUSI BATHOLOMEO NA CECILIA YAKAMILIKA

Bi. Harusi Mtarajiwa Cecilia na Bw. Harusi Mtarajiwa Batholomeo

Na Hassan Haji Ndunda

MAANDALIZI mazima ya Sherehe ya Harusi ya Bw. Batholomeo na Bi. Cecilia yamekwishakamilika kwa asilimia 99%. Nikizungumza na viongozi na baadhi ya wajumbe katika kamati hiyo teule wamesema kuwa sherehe imekamilika kwa asilimia 99% na kila kinachostahili kuandaliwa vimekwishaandaliwa na kukamilika.


Kikao cha Mwisho cha Kamati ya Maandalizi kilichokaa tarehe 23 Septemba' 2012 Msimbazi Centre Ilala Dar es Salaam


Katibu wa Kamati hii Bw. Norbert Nongwa akiongea kwa kujiamini alisema kuwa hatuna wasiwasi kuhusu maandalizi, kwa hivi sasa mambo yote yanakwenda vizuri na wageni waalikwa wakae katika mkao wa kusherehekea kwa furaha, kula kunywa na burudani kwa kwenda mbele.

Naye Mzee Augustino Kalinga alisema kuwa kwa kijana huyo tunataka kuonyesha kitu kipya kabisa, kwahiyo watu waje na nyoyo kunjufu kwa ajili ya burudani, kula, kunywa na kucheza bila wasiwasi wowote sisi ndio kina Kalinga.


Sherehe hii ya Harusi ya Bw. Batholomeo na Bi. Cecilia itafungwa tarehe 29 Septemba' 2012 katika Kanisa la St. Peter Oysterbay Jijini Dar es Salaam na kisha kufuatiwa na tafrija ya nguvu na ya aina yake itakayofanyika katika Ukumbi wa Deluxe Social Hall pale Sinza.

Kamati hii inaongozwa na viongozi mahiri na wasipenda utani katika kusimamia Sherehe nao ni:- Mr. Benard Ngulika akiwa ndiye nahodha (Mwenyekiti wa Kamati) akiratibiwa shughuli na Katibu Mr. Norbert Nongwa huku nafasi ya Mweka Hazina ikishikiriwa na Mrs Upendo Romanus Mtun'ge akisaidiana na Mr. Romanus Mtun'ge na nafasi ya Floor Manager ikikamatiwa na Mr. Erick Kaswaka

Kwa upande wa watenda kazi kamati imewatafuta ma - professional wa fani zao kama:- Mapambo na Chakula kutoka Deluxe Social Hall Sinza, MC wa Ukweee huyu si mwingine ni MC Luciana anayekwenda na muda na ma-Dj wa uhakika, Upande wa Kumbukumbu ukikamatiwa na mpigapicha mwenye professional kibao na uzoefu wa miaka isiyohesabika hapa namzungumzia Mr. Lutambi, Video akisimama Mr. Hassan Haji Ndunda kutoka Kampuni ya HVP Studio

Maharusi wakiwa Chuoni

 

 (Haji'z Video Production) picha zilizokwenda darasa, editing za uhakika ndio maana ikaitwa (The digital artist video professional) ndugu zangu kaeni mkao wa kubamba matukio na kamati imeshaahidi ni kula, kunywa, kucheza mpaka sweeeeee!

Post a Comment

0 Comments