BINTI AJA JUU KATIKA KUOGELEA

Agness Geofrey Kimimba

AGNESS GEOFREY KIMIMBA

Binti anayekuja juu hivi sasa hapa nchini Tanzania hususan katika mchezo wa kuogelea.

Agness anayechezea timu ya kuogelea ya Marine Tanzania Swimming Club yenye Makao yake Makuu Kigamboni katika Manispaa ya Temeke katika Jiji la Dar es Salaam, amekuwa ni binti mwenye jitihada kubwa katika mchezo huu pale anaposhiriki katika mashindano mbali mbali yaliyokwishafanyika ndani na nje ya nchi.

 

Ebu pitia Profile yake hapa chini:

Jina Kamili:         AGNESS GEOFREY KIMIMBA
Umri:                    10 Yrs
Jinsia:                  Female
Shule:                  Ufukoni Primary School Kigamboni Dar es Salaam

Mashindano aliyokwishashiriki:
- Mainland mara 3     - Funkys Masaki Dar es Salaam
                                      - Hopac Tegeta Dar es Salaam

- Championship x 3  - Funkys Masaki Dar es Salaam
                                      - Hopac Tegeta Dar es Salaam

- Uganda Invitation      - Kampala Uganda

- Open Championship - IST (International School of Tanganyika) Dsm

- Riding Star 2010       - Dar es Salaam

- CANA Zone 4            - Maputo Msumbiji

Medali:
Mpaka hivi sasa Agness Geofrey Kimimba ana jumla ya medali 32 zikiwa za Gold – 7, Silver – 14 na Bronze 11
 

Agness



Agness Geofrey Kimimba

Matarajio:

Agness ana matumaini makubwa ya kushiriki mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika mwaka 2016 katika staili ya Buterfly ambayo Agness alivunja rekodi ya Taifa kwa kuogelea kwa dk 40 na baadae akavunja rekodi nchini Uganda kwa kuogelea kwa dk 38 na kisha akavunja rekodi ya dk 35:29 katika mashindano ya CANA Zone 3 & 4 yaliyofanyika Maputo nchini Msumbiji.

 

Mashindano anayotarajia kushiriki hivi Karibuni ni:

- Mashindano ya Isamilo yatakayofanyika tarehe 10 – 11 Novemba’ 2012 kule jijini Mwanza.

 

- Na Uganda Invitation yatakayofanyika tarehe 12      Desemba’ 2012 Kampala nchini Uganda


Post a Comment

0 Comments