Na Sonyo Mwenkale
Mkazi
wa kitongoji cha Chang'ombee kijiji cha Kolang’a Kata ya Jaila, Wilaya
ya Kilindi mkoani Tanga aliyefahamika kwa jina moja la Mvenelo (30),
anadaiwa kumuua mkewe, Mwenjuma Digwele (25), kwa kumkata kichwa kwa
shoka akiwa na ujauzito wa miezi minane.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman
Liwowa, lilitokea Septemba 17, mwaka huu saa 7:00 mchana katika
kitongoji cha Chang’ombe.
Baadhi ya watu waliofika muda baada ya tukio hilo, walidai kuwa
walikuta kichwa cha mwanamke huyo kimetenganishwa vipande viwili.
"Hata madaktari waliokwenda, walilazinmika kufanya kazi ya ziada kushona
kichwa na kurudisha katika hali yake ya kawaida," alisema mmoja wa watu
hao ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Hata hivyo, alisema sababu za mauaji hayo hawazifahamu lakini inahisiwa
kuwa ni wivu wa mapenz na mtuhumiwa alitoroka baada ya kutekeleza unyama
huo.
Imedaiwa kuwa kabla ya mume huyo kufanya unayama huo, aliwaamuru watoto wake kuondoka pale nyumbani waende kucheza.
Hata hivyo, polisi wilayani Kilindi, wanalalamikiwa kwa madai ya
kuushindwa kuchukua hatua mapema kutokana na kudokezwa mapema na Afisa
Mtendaji wa Kata ya Jaila kuhusiana na kuwepo kwa mpango huo.
Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo, alisema: "Polisi Kilindi
wanastahili kubeba lawama, tukio lilitokea mchana lakini wao walifika
siku iliyofuata, wana nia mbaya na Serikali ya CCM, malalamiko dhidi yao
ni mengi.”
Naye Mkuu wa wilaya hiyo, Liwowa, alisema: "Tukio hili la mauaji
linasikitisha mno, mtu kumuua mkewe tena mjamzito inasikitisha sana."
CHANZO:
NIPASHE
0 Comments