Siku ya siku ndio imekwishawadia kwa wawili hawa kutimiza ndoto yao ya kufunga ndoa, ni muda mchache tu kutoka sasa. Pale katika Kanisa la Azania Front ndani ya Jiji la Dar es Salaam itakapofungwa ndoa takatifu mbele ya mazabau na kuwa mwili mmoja. Kisha Tafrija ya nguvu itaitimishwa pale Msimbazi Centre Ilala Dar es Salaam.
Ama kwa hakika tunawatakia ndoa njema iliyojaa amani na upendo tele katika maisha yao ya ndoa na mungu awabariki kwa kila jambo, sherehe isiwe na dosari.
Kamati kama ambavyo imejipanga basi mungu awape busara ya kutenda mema na wageni waalikwa waondoke na simulizi nzuri kama walivyojinadi viongozi wa kamati wakati wa kumalizia maandalizi ya sherehe hii.
0 Comments