NASOZ AJA JUU

NASOZ AJA JUU


Mwanamuziki Chipukizi  wa kizazi kipya aitwaye Nassoro Rashid Mohamed akijulikana zaidi katika fani kwa jina la "NASOZ" mwenyeji wa mkoani LINDI lakini akifanyia shughuli zake Kigamboni  jijini Dar es Salaam.


Msanii huyu kwa sasa ameibuka na kuja juu na vibao vyake matata na vinavyokwenda na wakati na vyenye kusisimua.


akiongea na mtayarishaji wa blog hii. NASOZ amesema kuwa amekwisha rekodi nyimbo zipatazo nane mpaka sasa na alizitaja nyimbo hizo kuwa ni:-


Sema na Moyo wako - aliomshirikisha msanii mkongwe wa bongo fleva Q-Chillah

aliourekodi METRO STUDIO kwa Producer Said Comorien na Allan Mapigo.


ukifuatiwa na "Usiondoke" aliomshirikisha pia Q-Chillah uliorekodiwa (BIG TIME Production) kwa Said Comorien bado video


mwingine ni "Niimbe Nini" alioimba yeye mwenyewe uliorekodiwa POTEZA RECORD kwa Said Fella (Mkubwa na Wanawe) video itatoka hivi karibuni


wa nne ni "Mvuvi" uliorekodiwa (TATUU RECORD) kwa Baba Baisa


wa tano unaitwa "KAWAPE SALAMU" ulioimbwa kwa maadhi ya mchiriku, uliorekodiwa (FABRIS RECORD)


na wa sita unaitwa "IMANI" aliomshirikisha mwanamuziki wa bongo fleva mkongwe SQUEZER uliorekodiwa (BAUCHA RECORD)


Nyimbo zote hizi ni moto wa kuotea mbali na ebu zisikilize  hapa chini.




kati ya hizi nyimbo moja ya "KAWAPE SALAMU" ishafanyiwa video na kampuni ya HVP STUDIO na Producer Hassan Haji Ndunda ndani ya HVP Studio (Haji'z Video Production iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam na tayari video hii inabamba katika chaneli kibao za luninga na chaneli ya TBC1 kipindi cha Ze Bang na vinginevyo ebu ipigie chabo hapa.




Post a Comment

0 Comments