Tanzania yatoa Salamu za Rambirambi Kifo cha Zenawi
Hayati Meres Zenawi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete asubuhi ya Agosti 21, 2012, amepokea kwa mshtuko
mkubwa, Masikitiko na Huzuni nyingi Taarifa za Kifo cha Waziri Mkuu wa
Ethiopia, Mheshimiwa Meles Zenawi, kilichotokea jana usiku nje ya Nchi
ambako alikuwa anatibiwa.
Kufuatia Taarifa hizo, Mheshimiwa Rais Kikwete, kwa niaba ya wananchi
wa Tanzania, Serikali yake na kwa niaba yake mwenyewe amemtumia salamu
za rambirambi Rais wa Ethiopia, Mheshimiwa Girma Wolde-Giorgis.
Katika rambirambi zake kwa Mheshimiwa Wolde-Georgis, Rais Kikwete
amesema”Tanzania imepokea kwa Mshtuko mkubwa, Masikitiko na Huzuni
nyingi Taarifa za kifo cha Mheshimiwa Meles Zenawi kilichotokea jana
usiku.”
“Kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, Serikali yangu na mimi mwenyewe,
natuma salamu zangu za dhati za rambirambi kwako, kwa Wananchi wa
Ethiopia na kupitia kwako kwa Mheshimiwa Azeb Mesfin, mjane wa
marehem”amesema Dk.Kikwete
0 Comments