Sasa hivi mwili wa
Marehemu upo katika Msikiti wa Sheahk Adhir,Kariakoo kwa ibada ya
Kusalia Mwili na baada ya Swala ya Ijumaa,Mwili utazikwa kwenye Makaburi
ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwili ukipakiwa kwenye gari.
Dua ikisomwa kabla ya kuondoka na Mwili wa Marehemu kwenda mazikoni.
Rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania,Saimon Mwakifwamba akimpokea Mbunge wa
Jimbo la Kigoma Kaskazini,Mh. Zitto Kabwe alipokuwa akiwasili msibani
hapo.
Waombolezaji wakiwa Msibani mapema asubuhi hii.
Pamoja
na kwamba kulikuwa na Mvua kubwa lakini hakuna alitaka kuondoka msibani
hapo mpaka pale mwili ulipoondoka kuelekea Msikitini kwa Kusalia na
baadae kwenye Mazishi.
Mwili ukiondoka nyumbani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na baba mzazi wa marehemu Sajuki
wakati wa mazishi ya msanii huyo leo katika makaburi ya Kisutu jijini
Dar es salaam
Jeneza lililobeba Mwili wa
Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) likiwasili kwenye Makaburi ya
Kisutu jijini Dar es Salaam mchana huu tayari kwa Mazishi yaliyoongozwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mh. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye Kaburi la
Marehemu Sadick Juma Kilowoko (SAJUKI) yaliyofanyika mchana huu kwenye
Makaburi ya Kisutu,Jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya
msanii Sajuki leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.Picha Na Ikulu
0 Comments