Mkongwe mwenye heshima tele kunako game la filamu za Kibongo, Jacob Steven alias JB ameanza kutusua kimataifa na sasa yupo mbioni kuhamishia makazi yake nchini Zambia.
Mwingizaji huyu ambaye pia ni Director wa movie chini ya kampuni yake ya A Jerusalem Company siku ya leo amechonga na BK Copkuhusiana
na kupata shavu kutoka kwa waandaaji wa filamu nchini humo na tayari
wameshakamilisha taratibu zote za yeye kwenda huko kwa ajili ya kufanya
kazi za sanaa.
Kuhusiana kitu ambacho kinamfanya mpaka sasa yupo nchini mkali huyu wa filamu kama “DJ Ben” na sasa “Ukurasa Mpya” alifunguka kwa kusema “Kinachonikwamisha
kwa sasa ni mkataba nilionao hapa Bongo, nikimaliza basi nitakwenda
huko kwa sababu masilahi ni makubwa zaidi ya hapa nyumbani,”
“Kimsingi nitahamia huko na familia yangu kabisa, pia
nitaongozana na wasanii wachache. Shughuli zote za filamu nitakuwa
nazifanyia huko. Kiukweli jamaa wamenipa dau kubwa sana, ni mara tatu ya
fedha ninayopata (kwa kila filamu) hapa nchini.” added JB.
0 Comments