TAARIFA ambazo zimetufikia muda huu ni kwamba
wananchi wenye hasira mkoani Mbeya wamefunga barabara eneo la Kwa Mama
John na kuzuia malori ya mafuta yanayosafarisha mafuta kwenda nchi
mbalimbali kupitia mkoa hiyo kwa kile kukasirishwa na wao kuwa na uhaba
mkubwa wa mafuta, ilhali nishati hiyo inapitishwa kwenda nchi jirani.
Taarifa zaidi zinasema wananchi hao wametishia kuchoma moto lori
lolote litakalo vuka eneo hilo. Mtandao huu unafuatilia tukio hilo kwa
karibu na tutaendelea kuwaletea taariza zaidi za tukio hilo.
0 Comments