kwa mujibu wa Mh. Mo Dewji blog, wasanii wa Bongo Movie ambao ni
maadhi ya mastaa maafuru nchini, Wema Sepetu na Aunt Ezekiel, wamekutana
na waandishi wa habari kwa lengo la kuomba radhi Watanzania kufuatia
picha za “utata” walizopigwa wakati wa Tamasha la Serengeti Fiesta
lililofanyika Dodoma. Picha hizo zilisababisha baadhi ya watu na blogs
kulalamika kwamba walikua wako “nusu uchi.”
“Kiukweli
hatujafurahia na tumeumia sana na tunatumia fursa hii kuomba Msamaha.”
Wema Sepetu alikaririwa akisema na Mh. Mo Dewji blog. Zifuatazo ni
baadhi ya picha za tukio hilo. Aunty Ezekiel alisisitiza kwamba wameumia
sana kwa kuonekana kwa picha zile kwa sababu wao kama wanawake katika
jamii, wana wazazi, Ndugu, jamaa, marafiki pamoja na mashabiki
mbalimbali wa kazi zao ambao wanawaheshimu kuliko baadhi ya watu
wanavyofikiria. Picha na habari kutoka :Mo Dewji Blog. Zifuatazo ni picha kutoka kwenye mkutano huo:
“Kiukweli hatujafurahia na tumeumia sana, na tunatumia fursa hii kuomba Msamaha.” – Wema Sepetu
Wema
Sepetu akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Msanii wa Bongo Movie
Aunt Ezekiel na kushoto Katibu Mkuu wa TAFF Wilson Makubi.
Aunt Ezekiel akizungumza na waandishi wa habari
Baadhi ya picha hizo zilizopelekea wasanii hao kuomba radhi. Pichani wasanii Aunty Ezekiel na Steven Nyerere (Kulia )
0 Comments