Wendesha mashtaka wanaochunguza
kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Palestina Yasser Arafat nchini Ufaransa,
watawasili mjini Ramallah ,katika Ukingo wa Magharibi mwezi ujao
kulifukua kaburi la Arafat.
Wachunguzi watafukua kaburi la Arafat ili kuifanyia uchunguzi wa kisayansi maiti yake.
Majasusi kutoka nchini humo tayari, wamemuhoji mjane wake Suha mjini Paris, ambaye anaamini kuwa alipewa sumu.
Ufaransa ilianzisha uchunguzi katika mauaji hayo
mwezi Agosti baada ya wataalamu nchini Uswizi, kupata chembechembe za
sumu aina ya (Polonium) kwenye nguo zake.
Arafat alifariki katika hospitali moja mjini Paris miaka minane iliyopita.
0 Comments