Mkurugenzi
wa Maendeleo na Utamaduni wa Wizara ya Habari Bw. Herman Mwasoka
(mwenye
suti nyeusi) akimfariji Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma
Kilowoko alipofika nyumbani kwa
marehemu kuhani msiba huo Tabata Bima
jijini Dar.(Picha zote na Mo Blog).
|
Mkurugenzi
wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya Habari
Bw. Herman Mwasoka akitia
saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu
Sajuki jijini Dar leo.
|
Msanii
mkongwe katika tasnia ya muziki wa Dansi na Rhumba Kikumba Mwanza Mpango
almaarufu kama King Kiki akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani
kwa
Marehemu Sajuki Tabata Bima jijini Dar leo.
|
Mzee King
Kiki akiteta jambo na Mkurugenzi wa Utamaduni na Maendeleo wa Wizara ya
Habari
Bw. Herman Mwasoka (katikati) nyumbani kwa marehemu Sajuki jijini
Dar leo. Kulia ni Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Bi. Joyce
Fisso
|
Wasanii
mbalimbali na wakiendelea kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki Tabata
Bima jijini
Dar es Salaam. Pichani ni Msanii wa muziki Dokii (kushoto)
sambamba na Mshiriki wa Shindano
la Big Brother Africa Mwisho Mwampamba
na wasanii wengine.
|
Mchekeshaji
maarufu wa The comedy Masanja Mkandamizi akijifuta jasho kwa mbali
akielekea msibani
nyumbani kwa Marehemu Sajuki. Masanja alikuwa ni mmoja
wa wahamishaji katika kuchangia
pesa za matibabu ya marehemu Sajuki
kwenda nchini India kupitia kipindi cha Luninga
cha The Comedy
kinachorushwa na Televisheni ya TBC.
|
Baadhi ya waombolezaji wakiwa kwenye huzuni kutafakari kifo cha Sajuki. |
VIONGOZI WA
SERIKALI WAKIWASILI: Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam,
ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu
kushoto)
akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mh.Iddi Azzan
wakipokelewa na
Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon
Mwakifamba na wasanii wengine wa filamu
baada ya kuwasili nyumbani kwa
Marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani msiba huo.
|
Mkuu wa
Itifaki Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimuongoza Mh.Makongoro
Mahanga
sehemu maalum kwa ajili ya kutia saini kitabu cha maombolezo.
|
Mbunge wa
jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na
Ajira,
Dk. Makongoro Mahanga akitia saini katika kitabu cha maombolezo
nyumbani kwa marehemu Sajuki.
|
Mbunge wa Kinondoni Mh. Iddi Azzan naye aliangusha saini kwenye kitabu hicho. |
Mzee King Kiki akizungumza jambo na Waheshimiwa Wabunge kwenye msiba wa Sajuki
Tabata Bima jijini Dar es Salaam leo. |
Waheshimiwa
wakielekea nyumba ya jirani walikokusanyika baadhi ya waombolezaji na
wasanii wa
filamu nchini kwa ajili ya kuzungumza machache na kutoa Ubani. |
Katibu wa
Fedha msibani hapo mchekeshaji maarufu Steve Nyerere akiwakaribisha
waheshimiwa
wabunge kuzungumza na hadhira ya waombolezaji (hawapo pichani). |
Mbunge wa
jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na
Ajira,
Dk. Makongoro Mahanga akitoa salamu zake za rambimbi na kuahidi kuchangia shilingi 200,000/= kwa ajili ya kufanikisha shughuli za mazishi ya mpendwa wetu Marehemu Sajuki atakayezikwa Kesho Ijumaa katika Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. |
Mbunge wa
jimbo la Kinondoni Mh. Iddi Azzani akielezea kwa majonzi alivyopokea
taarifa za
msiba wa Sajuki na kuahidi kushirikiana bega kwa bega na Wastara panapomajaliwa ya Mola katika malezi ya mtoto aliyeachwa na marehemu na kuwaasa wadau, ndugu, jamaa na marafiki kumsaidia Wastara kutokana na hali yake na amechangia kiasi cha Shilingi 500,ooo/= kufanikisha shughuli za mazishi ya marehemu Sajuki. |
Pichani Juu
na Chini ni Umati wa waombolezaji ukisikiliza nasaha za waheshimiwa
Wabunge
(hawapo pichani) walipofika nyumbani kwa marehemu Sajuki kuhani msiba huo. |
Kazi ya
kuosha vyombo si kina Dada tu, hata kina Kaka wanaweza pia…
.Pichani ni baadhi ya Watangazaji wa Clouds Radio wakiongozwa na Dina Marios kushiriki kuosha vyombo vilivyotumika katika msiba huo huku wakisaidiana na waombolezaji wengine. |
Mganga wa
Jadi anayefahamika kwa jina la Dokta Manyaunyau (kushoto) sambamba na
Msanii
wa filamu nchini Cloud wakisikiliza mawaidha ya waheshimiwa wabunge (hawapo pichani). |
Mkuu wa
Itifaki msibani hapo Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimpokea
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete alipowasili nyumbani kwa marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam. |
Mwenyekiti
wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw.
Ridhiwani Kikwete
akitoa pole baada ya kusaili kwa baadhi ya ndugu wa karibu wa marehemu Sajuki msibani hapo. |
Bw.
Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Baba mzazi wa marehemu Sajuki Mzee
Juma Kilowoko nyumbani
kwa marehemu Tabata Bima jijini Dar es Salaam. |
Mwenyekiti
wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw.
Ridhiwani Kikwete akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Sajuki leo |
.
Bw. Ridhiwani Kikwete akimpa maneno ya faraja Baba mzazi wa Marehemu Sajuki Mzee Juma Kilowoko. |
Bw. Ridhiwani Kikwete akitoa mkono wa pole kwa mke wa marehemu Sajuki Bi. Wastara (mwenye buibui). |
Bw. Ridhiwani Kikwete akimfariji mama mzazi wa Marehemu Sajuki alipofika nyumbani hapo kuhani msiba huo. |
Rais wa
Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akizungumza
machache
kabla ya kumkaribisha Bw. Ridhiwani Kikwete kuzungumza machache na waombolezaji. |
Mwenyekiti
wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw.
Ridhiwani Kikwete
akizungumzia marehemu Sajuki na kuwataka wanawake kuiga mfano wa Maisha ya Sajuki na Wastara jinsi walivyokuwa wakiishi na Upendo mpaka Umauti ulipomkuta marehemu Sajuki na kuwasisitiza kuenzi yale yote mema aliyokuwa akifanya kipindi cha uhai wake na kuwamasisha Umoja na Mshikamano baina yao. Bw. Ridhiwani Kikwete naye alichangia Shilingi 500,000/= kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu Sajuki anayetarajiwa kuzikwa Kesho Ijumaa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. |
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani). |
Marehemu
Sajuki alikuwa kipenzi cha watoto na wakubwa pia. Pichani ni Umati wa
watoto wanaokaa
jirani na Nyumba ya Marehemu Sajuki wakiwa wamekusanyika huku wakionyesha majonzi na simanzi tele. |
0 Comments